.

.

.

.

Tuesday, August 02, 2016

KITENGO CHA KUTOA HUDUMA YA MATANGAZO KWA KUTUMIA TEKNOLOGIA YA KIDIGITALI CHAZINDULIWA


Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (katikati) akimsifia msanii Diamond Platinumz kwa jinsi ambavyo amekuwa akiitangaza Tanzania nje ya nchi kwa muziki wake.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga alielezea machache mbele ya wageni na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo juu ya huduma mpya ya matangazo katika bara la Afrika utakaowanufaisha watangazaji, wasanii na watu maarufu uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel na Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Binary, Eni Kihedu. 

Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabrielakimsifia Wema Sepetu jinsi ambavyo amekuwa akilitunza jina lake.
Msanii Diamond Platinuz akitoa shukrani zake za pekee kwa niaba ya wasanii walihudhuria hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga (kushoto) akizunguza na Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel wakati wa uzinduzi wa huduma ya matangazo kutumia teknolojia ya kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara kutangaza biashara zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni ni
Wageni waalikwa waliohudhuria shughuli hiyo.
Wasanii waliohudhuria shughuli hiyo.
Waandishi nao hawakuwa nyuma kufuatilia tukio.
Huduma ya matangazo kidigitali kwa kutumia wasanii na watu maarufu yaanzishwa nchini.


KAMPUNI inaoongozwa kwa kutoa huduma ya matangazo ya biashara nchini ya Aggrey & Clifford imezindua kitengo cha kutoa huduma ya matangazo kutumia teknolojia ya kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara kutangaza biashara zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika jamii ambayo itanufaisha pande zote zitazoshiriki kutumia huduma hii .



Huduma hii ya kisasa inayoendana na wakati wa sasa wa kizazi kipya inawezesha matangazo kuwafikia walengwa wengi na kwa haraka inasimamiwa na kampuni tanzu ya masuala ya huduma za matangazo ya biashara kwa kutumia teknolojia ya kidigitali ya Aggrey&Clifford inayojulikana kama Binary.

PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.

No comments:

Post a Comment