Mama mmoja mwenye ulemavu wa ngozi yaani albino, ambaye pia ni mjamzito, amevamiwa na watu watatu akiwemo jirani yao usiku wa manane na kumfyeka mikono. Majeruhi huyo aliyefahamika kwa jina la Bi.Mariamu Stanfod amesema kuwa akiwa amelala na wadogo zake, alivamiwa na wahalifu hao kisha wakamkata mikono na kutoweka. Amesema kutokana na kupoteza mkono, sasa anahitaji msaada hasa utakapofika wakati wa kujifungua na jinsi ya kumhudumua mototo wake. Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali Tteule ya Mrugwanza ambayo amelazwa majeruhi huyo, Dk. Maginus Ndolichimpa, amesema mwanamama huyo alikatwa na kitu chenye ncha kali. Akasema kitu kilichotumika kumkata mikono kilikuwa na kutu inayoozesha vidonda, hali inayowalazimisha kusafisha vidonda hivyo kila siku ili kumnusuru majeruhi huyo na kansa ya mifupa. Baba mzazi wa Marimu, Bw. Stanfod Bandaba amesema, baada ya kushitushwa na kelele za mtoto wake aliyekuwa akiomba msaada, alitoka nje na kuwakuta wahalifu hao wakiwa wamezingira nyumba yake. Amesema hata hivyo wahalifu hao walifanikiwa kutoroka ila kutokana na maelezo ya Mariamu wameweza kubaini mmoja ni jirani yao. Bw. Bandaba amesema wananchi walifanikiwa kumtamata jirani huyo akiwa nyumbani kwake na kumfikisha kituo cha Polisi. Amesema kwa yeyote atakayegushwa na tukio na angependa kumsaidia Bi. Marimu, atumie akaunti namba 3211601173 au awasiliane na Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo kwa simu namba 0785-424299, au 0755- 8019 17.
No comments:
Post a Comment