.

.

.

.

Tuesday, November 11, 2008

EPA HAIEPEKI NDULLU ATAJWA

Wakati watuhumiwa wa wizi wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje, EPA, wanazidi kuongezeka, sakata hilo limechukua sura mpya baada ya kuibuka kwa madai mapya yanayomhusisha gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu. Katika madai hayo, inaelezwa kuwa Profesa Ndullu aliyenyaka nafasi hiyo baada ya gavana aliyekuwepo, Dk. Daud Balali ambaye sasa ni marehemu kutimuliwa kazi, hakustahili kushikilia nafasi hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mmoja wa waliokuwa wasaidizi wa Balali aliyeboronga hadi mapesa hayo yakabebwa kiulaini. Aliyeibua madai hayo ni Mbunge wa jimbo la Karatu, Dk. Wilbroad Slaa. ``Binafsi nilishangaa kuona Prof. Ndullu akipandishwa cheo na kuwa gavana mpya... ikumbukwe kuwa mapendekezo ya kampuni iliyokagua na kubaini wizi huo wa pesa za EPA ( Ernst & Young), yalitaka safu nzima ya uongozi wa BoT ibadilishwe,`` akadai Dk. Slaa. Akadai kuwa kwa vile Prof. Ndullu alikuwa miongoni mwa safu hiyo, hakupaswa kupewa ugavana. Sambamba na hilo, Dk. Slaa amedai kuwa bado hajaridhishwa na watu walioburuzwa mahakamani kwa kile alichodai kuwa, anaamini wapo vigogo wanaostahili kuunganishwa na watuhumiwa hao katika kesi zinazowakabili. Akadai kuwa kwa anavyoamini yeye, wafanyakazi wa BoT walioshitakiwa katika kesi hiyo hadi sasa, ni baadhi tu ya watuhumiwa wa sakata hilo, kwani vigogo wa kweli walioidhisha fedha hizo hadi zikaweza kuchotwa kwa kiwango kilichotajwa bado hawajaguswa.

No comments:

Post a Comment