.

.

.

.

Sunday, November 02, 2008

MWENYEKITI AU MBIONI KUTAFUTA UFUMBUZI WA DRC

MWENYEKITI wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa umoja huo uko tayari kuongoza jitihada za kutafuta amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye uwanja wa ndege wa zamani wakati wa kuwasindikiza mawaziri wa mambo ya nje David Milliband wa Uingereza na Bernard Kouchener wa Ufaransa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe alikiri kuwepo kwa hali ngumu ya kimaisha inayosababishwa na vita vya wenywe kwa wenyewe nchini humo.
"Mwenyekiti wa AU Rais Jakaya Kikwete anatarajia kuitisha kikao cha haraka kitakachowahusisha viongozi wa Afrika, kwani tayari wameshaliona jambo hilo kuwa ni tatizo na ili kuwanusuru wananchi wa Kongo, lazima pande mbili zinazovutana ziridhie makubaliano yaliyosainiwa Nairobi," alisema Waziri Membe.
Rais Kikwete pia alisisistiza kuwa ipo haja ya kuchukuliwa kwa hatua za haraka kuepukana na uwezekano wa kuzuka kwa janga na zahama kubwa ya kibinadamu kutokana na kudorora kwa hali ya usalama katika eneo hilo, hasa katika eneo la Kivu Kaskazini, ambako waasi wanapambana na majeshi ya Serikali.
Mwenyekiti huyo ameeleza msimamo huo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe mzito wa mawaziri wa nje wa Uingereza na Ufaransa ambao walikuja kumwona Ikulu, Dar es Salaam, jana

No comments:

Post a Comment