Kampuni ya ndege ya ATCL imesitisha safari zote za dege kubwa lililogharimu mabilioni ya shilingi kulikodi kutokana na hali mbaya ya ukata kwenye shirika hilo ambalo linatarajiwa kubinafsishwa/kuingia ubia na kampuni ya Kichina. Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika hali katika shirika hilo ni mbaya na hasa vitendo vya kifisadi vinavyohusisha matumizi mabaya ya fedha kidogo waliyonayo.
Uchunguzi unaonesha kuwa marubani wa kigeni toka Ufaransa ambao ndio walikuwa warushe ndege hiyo wamegoma kufanya hivyo baada ya kugundua kuwa haikuwa katika hali ya kuweza kusafiri angani kutokana na kasoro ya kifaa fulani ndani ya ndege hiyo ambayo ilipigiwa debe kuwa ni "future ya ATCL". Marubani hao ambao wanalipwa maelfu ya dola wamekuwa wakiishi kama wako kwenye mapumziko ya muda wa kiangazi (summer vacation) kwani Mkataba wao unawalipa fedha wawe wanarusha ndege au la.

No comments:
Post a Comment