Msanii Juma Kassim Nature aliyekuwa akishikiliwa na watoto wa IGP Mwema,kwa tuhuma za kula uroda na mwanafunzi anayedaiwa kuwa na umri chini ya miaka 18, ameachiwa wa dhamana.
Hayo yalithibitishwa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Temeke, Emmanuel Kandihabi lakini hakufafanua vigezo vilivyotumika kumwachia msanii huyo. Kwa mujibu wa kamanda huyo kama ikibainika dhamana kwa msanii huyo ilitolewa kimakosa, basi ataingilia kati kufuatilia suala hilo kutoka kwa mkuu wa kituo alichoshikiliwa kabla ya kuachiwa. Hata hivyo habari tulizozipata kutoka maskani ya kundi lake Wanaume Halisi Temeke..zilidai kuwa mama yake Juma Nature akishirikiana na majirani zake ndio waliomdhamini msanii huyo. Nature alikuwa anashikiliwa kwenye Kituo cha Mbagala Kizuiani tangu Jumapili kabla ya kuachiwa kwa dhamana jana.

No comments:
Post a Comment