.

.

.

.

Wednesday, December 24, 2008

WATOTO WA KIMASAI WAUWAWA KWA MABOMU

Watoto wanne wa Kimasai wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya kulipukiwa na bomu katika kijiji cha Embukoi karibu na eneo la kambi ya mafunzo ya Jeshi la polisi Kilelepori wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro. Wakizungumza jana katika eneo la tukio wananchi wa kijiji hicho wamelaani kitendo kilichotokea kwa madai kuwa wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu katika serikali ya mkoa bila mafanikio. Wamesema kuwa wameshapeleka malalamiko yao Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bwana Mohamed Babu kuhusu madhara yanayowapata. Madhara hayo ni pamoja na mifugo yao kuuwawa pamoja na wanawake wajawazito kuharibika mimba na wazee kupata mishtuko na kufariki dunia kutokana na mabomu na silaha za moto zinazopigwa katika kambi hiyo ambayo iko katika makazi ya watu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Bwana Lucas Ng`hoboko amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amewataja watoto hao kuwa ni Larta Lota, Samweli Julius, Liyomomo Olikirima na Rose Saningo na majeruhi ni Isaya Ndiogi ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa matibabu. Miili ya maiti za watoto waliofariki ikiwa katika bonde la kijiji cha Embukoi mara baada ya kulipukiwa na bomu katika bonde la mlima Embukoi uliopo wilayani Siha mkoani Kilimanjaro. Bomu hilo lilikuwa likitumiwa na askari polisi wakati wa mazoezi ya shabaha katika mlima huo.(KUMRADHI KWA PICHA HII YA MASIKITIKO)

No comments:

Post a Comment