.

.

.

.

Tuesday, May 19, 2009

YANGA MAN U YA TZ

KLABU ya YANGA ndiyo inayoongoza kwa kuingiza mapato mengi zaidi kuliko timu yoyote nchini.
Katika Ligi Kuu Bara iliyomalizika hivi karibuni, Yanga inakadiriwa kuingiza mapato ya zaidi ya shilingi bilioni moja kutoka katika na vyanzo mbalimbali msimu huu.
Kwa kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara pekee Yanga imeingiza shilingi milioni 62 kutoka kwa wadhamini Vodacom na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro.
Yanga wamepokea kitita cha shilingi milioni 37 kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, pamoja na Sh 25m za ubingwa kutoka TBL.
TBL inaidhamini Yanga kwa sh 800m kwa mwaka, huku kila mwezi wakiwapatia Sh16m.
Mbali na fedha hiyo, Yanga imekuwa ikiingiza mapato makubwa katika mechi zake mbali mbali za ligi na kimataifa kupitia mapato ya milangoni kwa viingilio vya mashabiki.
Katika mechi dhidi ya Al Ahly, Yanga walivuna shilingi milioni 100 ikiwa ni mapato ya mlangoni, huku wakilipwa na klabu hiyo ya Misri, 15m kwa ajili ya matangazo ya televisheni na matangazo ya mabango uwanjani.
Katika mechi zake mbili dhidi ya watani wake wa jadi Simba, mabingwa hao wamefanikiwa kupata zaidi ya milioni 97. Mchezo wa kwanza wa livuna Sh milioni 50 na mechi ya marudiano Sh 47m mechi zilizochezwa kwenye Uwanja wa Taifa.
Timu hiyo ya mtaa wa Twiga na Jangwani pamoja na kupata fedha hizo bado inapata udhamini mnono wa Yusuf Manji ambaye haijulikani anachangia kiasi gani kwa mwaka katika klabu hiyo, lakini amekuwa akimwaga fedha kila kukicha.
Manji amefadhili ukarabati mkubwa wa jengo la klabu hiyo pamoja na Uwanja wa Kaunda ambao uongozi wa Yanga umedai unataka kutumia katika baadhi ya mechi za ligi kuu msimu ujao.

No comments:

Post a Comment