
Alisema kuwa marehemu aliamuka salama leo na kuendelea na shughuli zake za kila siku ofisini kwake mpaka majira ya saa 4:00 asubuhi ambapo alizidiwa ghafla na kukimbizwa Hospitali ya rufaa ya Bugando.Habari kutoka katika ofisi ya aksofu huyo, zimeeleza kuwa alipatwa na maradhi hayo wakati akiwa katika maandalizi ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Vatican ambaye alikuwa akitarajiwa kufanya ziara jimboni kwake Oktoba 5 mwaka huu kwa ajili ya kufungua ujenzi wa hospitali ya watoto.“Baada ya kufikisha hospitalini hapo madaktari waliahangaika kuokoa maisha yake lakini nahati mbaya lifariki dunia majira ya saa 8;30 mchana,” alieleza Padri Revocatus Makonge.
Askofu Mayalla alizaliwa Aprili 23 mwaka 1940 katika katika kijiji cha Nera wilayani Kwimba na kupata elimu yake ya msingi katika wilaya hiyo na masomo ya sekondari.Askofu Mayalla alikuwa amehitimu shahada ya kwanza ya elimu aliyopita katika chuo kikuu cha Loyola huko Chicago Marekani mwaka 1973 hadi 1975. Frederick Katulanda, Mwanza.
No comments:
Post a Comment