.

.

.

.

Saturday, September 18, 2010

MTOTO WA RAIS JK AZIDI KUNG'ARA CCM


Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM, Ridhiwani Kikwete akihutubia katika mkutano wa ndani katika Kijiji cha Kilanjelanje Jimbo la Kilwa Kaskazini, ambapo aliposimama kwa muda kuwasalimia wanachama na kuwaeleza utekelezaji wa Ilani yao pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM, Ridhiwani Kikwete akiangalia ngoma ya utamaduni wakati kikundi cha Siasa Makondeko alipowasili kwenye mkutano ulioitishwa na Mgombea ubunge wa jimbo la Mchinga kupitia CCM, Said Mtanda.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM, Ridhiwani Kikwete akihutubia katika mkutano wa hadhara juzi katika Kata ya Kilangala ulioandaliwa na Mgombea ubunge Jimbo la Mchinga, Said Mtanda wilayani humo juzi.Ridhiwani ameambatana na baadhi ya vijana makada kwenye ziara hiyo ya kupanga mikakati ya ushindi mkubwa wa CCM.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM, Ridhiwani Kikwete (katikati) akiondoka kutoka kwenye mkutano baada ya kuwahutubia wananchi jana katika Kata ya Kilangala,Dar es Salaam juzi.Kulia ni Mgombea ubunge wa jimbo hilo, Said Mtanda.

No comments:

Post a Comment