.

.

.

.

Tuesday, January 11, 2011

MZEE "KIDUME CHA MBEGU"


MWANAMME mmoja mwenye umri wa miaka 94 na mkewe ambaye ana umri wa miaka 52 aitwaye Shakuntala, hivi sasa wamesimamisha kawaida yao ya kufanya mapenzi mara tatu kwa usiku mmoja na kuelekeza mawazo yao katika kumtunza mwanao wa kiume akitwaye Vikramjeet.

“Nina afya njema na nafurahia ngono na mke wangu. Ni muhimu kwa mume na mke kufanya mapenzi kila mara,” Raghav, mwenyeji wa Haryana kaskazini mwa India aliliambia gazeti la The Sun.

Aliongeza: “Kila wakati mke wangu akiniomba kufanya mapenzi tunafanya usiku mzima, lakini hivi sasa nimeacha tabia hiyo ili tumtunze mwanetu.”

Mke wake anasema kwamba hafikirii mumewe ni mzee sana, akaongeza: “Anaweza kufanya mapenzi kama mtu mwenye umri wa miaka 25 na akaendelea usiku mzima. Ni mwanamme wa ajabu.”

Wanandoa hao wamedokeza kwamba baada ya kuhakikisha malezi bora ya mtoto wao, wanafikiria kutafuta mtoto wa pili.

Raghav, ambaye alikuwa mcheza mielekea wakati wa ujana na ambaye bado anafanya kazi kwa muda wa masaa tisa shambani akilima, ana imani atashuhudia mtoto wake akikua, na akawaambia waandishi wa habari kwamba watakapoitembelea familia yake baada ya miaka kumi watamkuta akiwa hai.

Mtu huyo amevunja rekodi ya kuwa mwanamme aliyepata mtoto akiwa na umri mkubwa zaidi duniani.

Ameivunja rekodi hiyo ambayo ilikuwa inashikiliwa na mkulima wa India, Nanu Ram Jogi, ambaye mke wake alizaa mtoto wa 21 wakati akiwa na umri wa miaka 90 mwaka 2007.

Hapa Uingereza, mwanamme ambaye alipata mtoto akiwa na umri mkubwa zaidi ni Raymond Calvert ambaye alikuwa na miaka 79 na ambaye mkewe alimzaa mtoto huyo akiwa na umri wa miaka 25 mwaka jana.

No comments:

Post a Comment