.

.

.

.

Thursday, November 03, 2011

SUALA LA USHOGA TANZANIA ...........

TANZANIA imekataa masharti ya Uingereza inayotaka nchi zinazotaka misaada yake ziruhusu vitendo vya ushoga. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe alitoa msimamo huo leo Jijini Dar es Salaam akisema huko ni kwenda kinyume na sheria na utamaduni wa nchi yetu inayotambua ndoa ya mme na mke kama kiini cha familia.

"Nchi yetu inaheshimu sheria na utamaduni wake hivyo hatupo tayari nchi nyingine kutuwekea masharti kama hayo ya kuwa na uhusiano wa jinsi moja, hili ni tamko hatarishi linaloweza kuvunja uhusiano na nje", Waziri Membe aliwaambia waandishi wa habari. Alisema tamko hilo ni msimamo wa chama cha Conservative na kibaya zaidi linatoka Uingereza ambako ndio wenye Jumuia ya Madola hivyo linaweza kusababisha kuvunjika kwake na Cameroun na nchi hiyo ndio watawajibika jumuia hiyo ikivunjika.

Alisema miongoni mwa nchi 54 za Jumuia ya Madola kati yake nchi 13 ushoga ni sehemu ya katiba yao wakati 41 hazina utamaduni huo hivyo msimamo wa Tanzania ni kuwa na ndoa za jinsi mbili tofauti, kinyume na hapo unafungwa kifungo miaka 30. Alisema kuendelea kukumbatia ushoga si jambo zuri na si la kulishabikia hata kidogo vinginevyo wanaweza kujuta nchi ikijihusisha na ushoga na kuukubali kupata misaada ya maendeleo.

"Tanzania hatuwezi kuyumbishwa kwa masharti ya kipuuzi bora tuitunze nchi yetu. Tanzania ni nchi maskini lakini kamwe haturuhusu kuingiliwa na nchi nyingine. Kama ndio hivyo basi wakae na hela zao," alisema Waziri Membe wizarani kwake.

Alisema katika mkutano wa Madola, walijadili mabadiliko ya hali ya hewa ambapo walibainisha nchi zinazotegemea mvua zichukue hatua gani kuishi bila kuathiri hali hali ya hewa. Pia alisema walijadili kuhusu hatua za kuchukua ili kuvisaidia visiwa vidogo kama Maldives vinavyoliwa na maji ya bahari yanayojaa kufuatia mabadiliko ya hali ya hewa. Alisema watakuwa na mkutano London Aprili mwakani kujadili mikakati hiyo.

2 comments:

  1. NDIYO Waziri mimi ni raia wa TZ na kuunga mkono kwa msimamo wako na naimani kabisa hatutalala njaa kwa sababu ya hiyo misaada inayotoka nje hiyo miaka yote ya nyuma hatukuwa na maadili hayo na hamna matatatizo yoyote nashukuru sana kwa uamuzi huo na tusimame kidete kwa msimamo wetu kwa sababu mataifa ya lioendelea wameruhusu hayo na kuharibu maadili ya ndoa ya mume na mke ni mambo ya kusikitisha sana na inabidi kuiombea dunia na kizazi kijao kwa uharibifu.Hongera waziri nakupa asilimia mia mbili kwa jambo hilo na MUNGU IBARIKI TZ NA WATU WAKE KUWA IMARA HAYO NI MAMBO YA AIBU NCHINI KWETU.

    ReplyDelete
  2. Ni lazima nchi yetu iwe na misimamo kwani hata hiyo misaada wanayotutisha nayo ni madini yetu wanayoyachukuwa na kujidai wanatusaidia wakati ni mali zetu walizozipeleka huko.TENA HAO MASHOGA WACHACHE WALIOPO HAPA NI KUWACHAPA FIMBO KILA TUTAKAPOWAONA.

    ReplyDelete