.

.

.

.

Tuesday, April 02, 2013

UNYAMA WA AJABU MKOANI MBEYA


MATUKIO ya kutisha na ya kinyama dhidi ya watoto wadogo yameendelea kuutikisa Mkoa wa Mbeya, baada ya mwanafunzi wa chekechea, Ayoub Agen (6) kuuwa kwa kuchinjwa mithili ya kuku na wauaji kuondoka na kichwa chake.
Hata hivyo wananchi wenye hasira walifanikiwa kumnasa mmoja wa watuhumiwa wa tukio hilo, ambaye hata hivyo jina lake halikuweza kupatikana ambapo baada ya kummbana ili aeleze sehemu  walikokificha kichwa cha marehemu aligoma hivyo kuamua kumteketeza kwa moto.
Habari za uhakika kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Ijoka  katika kata ya Mpombo, wilayani Rungwe, Rafael Mwaikenda,  zinadai kuwa tukio hilo lilitokea Machi 31 majira ya saa 11:00 jioni.
Akifafanua zaidi Mwenyekiti  huyo alisema,  marehemu Agen alikuwa ni mwanafunzi wa chekechea katika shule ya msingi Lusanje kijijini hapo na kwamba alikutwa na mauti hayo ya kikatili baada ya watu hao wasiofahamika kufanikiwa kumuiba nyumbani kwao.
Mwaikenda alisema  mwili wa marehemu uliokotwa ukiwa umetenganishwa kichwa na kiwiliwili huku kichwa kikiwa hakionekani hadi sasa ikiwa ni muda mfupi tu baada ya watu hao wasiofahamika kumwiba toka nyumbani kwa wazazi wa marehemu .
“Marehemu alichukuliwa na watu hao wasiofahamika akiwa anacheza na wenzake na wenzake baada ya kuona hivyo waliamua kutoa taarifa ambapo muda mfupi walianza kumtafuta bila mafanikio, lakini wananchi wakiwa wanaendelea na harakati hizo waliukuta mwili huo ukiwa umetelekezwa kichakana na wauaji hao kuondoka na kichwa” alifafanua Mwaikenda.
Mkazi mwingine katika kijiji hicho, Tumpale Sankemwa, alikielezea mkasa huo, alisema baada ya wananchi kugundua mwili huo wa marehemu waliendelea kuwasaka wahusika na wakiwa katika harakati hizo ghafla walikutana na mtu mmoja ambaye walimtilia mashaka.
Alisema baada ya kumfanyia mahojiano ya kina kwa kuwa alikuwa hafahamiki na mgeni kijijini hapo, alikuwa akijibu jeuri hivyo kuwapandisha hasira wananchi jambo lililosababisha kuanza kumshambulia na hatimaye kumuua papo hapo.
Hata hivyo alisema wakati wananchi wakiendelea kumshushia kipigon mtu huyo licha ya kutotaja jina lake, alikiri kuhusika katika tukio hilo kwa kueleza kuwa waliohusika walikuwa watatu na kwamba wenzake walikuwa wameondoka.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Kamishina Msaidizi wa jeshi la polisi,Diwani Athumani, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hadi sasa kichwa cha marehemu huyo hakijaonekana  na jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi.
“Ni kweli tukio hilo limetokea, hata hivyo mtu anayetuhumiwa kushiriki mauaji hayo naye aliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira  ambao licha ya kumuua waliuteketeza mwili wake kwa moto”.
Aliongeza kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo ni mwanaume anayekadiliwa kuwa na miaka kati ya 30 hadi 35  na kwamba uchunguzi wa awali umeonesha chanzo cha mauaji hayo kinahusishwa  na imani za kishirikina.


No comments:

Post a Comment