.

.

.

.

Friday, March 06, 2015

AZAM TV YAZINDULIWA RASMI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mmiliki wa Azam TV ambayo ni kundi la makampuni ya SS Bakhresa, Said Salim Bakhresa, (watatu kushoto waliokaa), waziri wa habari, utamaduni, vijana na michezo, Dkt. Fenella Mukangara, (katikati aliyejifunga kitambaa), naibu mkurugenzi wa Azam TV, Tido Muhando, (wakwanza kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa TV hiyo mara baada ya Rais kuizindua rasmi Ijumaa Machi 6, 2015. TV hiyo yenye studio zake, barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam, ni maarufu kwa vipindi vya michezo hususan soka


Rais Kikwete, akiwa ameketi na Mwen yekiti wa makampuni ya SS Bakhresa, Said Salim Bakhresa


Rais akiwa kwenye mahojiano na nabu mkurugenzi wa TV hiyo, Tido Muhando


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa fundi mitambo Mkuu wa Azam TV, Mehdoub al Hadad  juu ya namna gari la kurusha matangazo nje ya studio (OB Van) linavyofanya kazi wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mwenyekiti wa SS Bakhresa, Said Salim Bakhresa na wafanyakazi wengine wa TV hiyo


Said Salim Bakhresa, (kushoto), akimpa maelezo Rais Kikwete.

No comments:

Post a Comment