.

.

.

.

Thursday, September 25, 2008

UMEME UKANDA WA NBI


WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema moja ya changamoto zinazokabili nchi za ukanda wa Bonde la Mto Nile (NBI), ni kuongeza zaidi idadi ya watumiaji wa nishati ya umeme.
Akifungua mkutano wa pili wa mawaziri wa nishati kutoka nchi za NBI, Pinda alisema katika nchi hizo, watu wake wanaopata nishati hiyo ni asilimia 10.
Pinda alifafanua kwamba, nchi za NBI zinahitaji usambazaji na upatikanaji wa nishati ya kutosha ya umeme na ya kuaminika.
"Nchi za ukanda wa Nile zinahitaji umeme wa kutosha na kuaminika ili kuweza kufikia mahitaji yao ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii," alisema waziri mkuu.
Alisema jambo la msingi ni nchi hizo kuunganisha nguvu zao za rasilimali kwa pamoja, na kuangalia vyanzo mbadala ili kuviendeleza.

No comments:

Post a Comment