.

.

.

.

Thursday, April 30, 2009

LA MGAMBO READING

Kwa mara ya kwanza Afrika Jambo Band watawasha
moto siku ya jumapili ndani ya READING
03/05/2009 bank holiday weekend time 10pm till
3.45am entry £10@the door £7 in adv come early and


enjoy (bbq)
nyama choma&the best tunes with finest djs richie,peter,chambie,andy&eric
tule tunywe tucheze wote mnakaribishwa

CLOUDSFM NA LEO TENA

Watangazaji mahiri wa Clouds Fm 88.4 kupitia kipindi cha Leo Tena kinachorushwa kila siku ya jumatatu kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana.
Kutoka shoto ni bibie Gea Habib ambaye anakamua kipande kiitwacho heka heka,
kati ni Zamarad Mketema ambaye anafanya kipande cha Bongo Movie
pamoja na mama lao anaendesha kipindi kizima cha Leo Tena, Dina Marious wakiwa wamepozi na mwana wa Clouds Mwingine aitwaye
Athuman a.k.a Suka

Wednesday, April 29, 2009

SPOTTED

Usher spent the day with his adorable 17-month-old son Usher Raymond V in South Beach on tuesday with some friends.
While wife Tameka Foster –who nearly died while undergoing plastic surgery in Brazil last year — remained home to take care of their infant son Naviyd Ely Raymond, the father-son duo enjoyed some beachside male bonding before enjoying a picnic under the sun.
Sure, it’s cute now but it won’t be too long before Usher Jr. starts stealing all the lady attention away from Usher Sr.
Alicia Keys on a nightout yesterday.

KATUNI YA LEO


HII IMEKAAJE ???

Yusuf Manji (pichani), yule aliyetajwa na Reginald Mengi kama fisadi papa amefungua kesi ya kashfa, akimtaka Mengi amlipe Sh 1 (moja) kama fidia.
Kesi hiyo imefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kupitia kwa kampuni ya uwakili ya Muganda, Kamugisha na Bwana, lengo likiwa kutaka kusafishwa. Wengi wameipa tafsiri tofauti kesi hiyo; je, Sh 1 ndiyo thamani ya Manji; je, Mengi hana uwezo wa kumfidia Manji; au, Manji hana shida na pesa, bali kusafishwa.

KAMA ILIYOANDIKWA NA www.lukwangule.blogspot.com

HALI katika hospitali ya wilaya ya temeke ni ya kutisha, kutia huzuni na pia kusikitisha.Madaktari na wauguzi wamekuwa wakichemka vikali kusaidia wagonjwa mbalimbali waliotokana na milipuko ya mabomu katika kambi ya jeshi Mbagala.Dk Mahita alimwambia mwandishi wa habari hizi ambaye naye alifika hospitalini hapo pamoja na kuandika habari kuangalia watoto wake ambao mpaka jioni walikuwa hawajulikani walipoalisema kwamba mpaka saa kumi na nusu kulikuwa na majeruhi zaidi ya 155 waliofikishwa katika hospitali hiyo wengi wao wakiwa na hofu na kuzimia.Aidha Dk Mahita alisema mpaka muda huo alikuwa na maiti watatu mmoja akiwa mtoto.Ingawa alisema kwamba kila kitu kinaendelea vyema lakini ni wazi idadi ya wauguzi na kasi yakuingia kwa wagonjwa ilionyesha kuwaelemea wauguzi wa hospitali hiyo kiasi cha mkuu wa mkoa William Lukuvi aliyefika hapo kuamua kupiga simu kuomba msaada.Huku maelfu ya wananchi wakiwa wanaendelea kumiminika katika hospitali hiyo na kuzuiwa navikosi vya askari wa kutuliza ghasia wakisaidiwa na mbwa,magari ya kubeba wagonjwa na ya watu binafsi yalikuwa yakiingia na kutoka.Wengi walikuwa wameletwa wakiwa na hali mbaya ya mfadhaiko wengine wakiwa kama wamepigwana shoti.Mmoja wa maiti inadaiwa kwamba alikatwa vipande viwili na mabomu.Kitu ambacho kilionekana dhahiri katika mapokezi ni udogo wa sehemu hiyo ambapo ilikuwa nuikupokea wagonjwa kuangalia wana nini kuwapiga dripu na kisha kuwakimbiza.Dk mahita alisema kwamba walikuwa wanafanya mipango ya kupata eneo jingine la kutunza wagonjwa kwani hospitalini hapo palikuwa pamejaa.Watu waliokuwa wanataka kuwaona wagonjwa wao wa kawaida hospitalini hapo walishindwa kuingia katika hospitali kutokana pilikapilika za majeruhi na hofu ya usalama kwamba wakiruhusu maelfu ya wtau waliopo nje wanaotafuta ndugu na watoto watavamia hospitali na itakuwa taabu kubwa kuwaondoa.Mkuu wa mkoa katika mazungumzo na mwandishi wa habari hizi amesema kwamba moto umedhibitiwa katika hanga ambako mambomu yamelipuka ingawa anasema kwamba hawawezi kuwa na uhakika wa fukuto lililopo.Hata hivyo amesema hanga jingine ambako kuna makombora lipo salama.Serikali ilikuwa inatarajia kutoa taarifa yake jana jioni.Zifuatazo ni picha mbalimbali nilizopiga hospitali ya Temeke.

MITAA YA BONGO LEO BAADA YA MABOMU KULIPUKA











BREAKING NEWS !!! BONGO YAPATA UPEPO WA GAZA

WAKAZI WA MBAGALA WAKIWA KATIKA MTAFARUKU WA AINA YAKE
ENEO la Mbagala limetangazwa eneo la hatari kutokana na milipuko ya mabomu katika kambi ya kijeshi iliyopo huko.Kamanda Kova amesema kwamba watu hawaruhusiwi kwenda Mbagala na waliobaki huko wakwepe kukusanyika au kukaa chini ya maghorofa.Pia kamanda kova amesema wakuu wa vyombo vya kijeshi na usalama wameelekea eneo la tukio na kuthibitisha kwamba tayari watu wanne wamekufa katika milipuko hiyo.mapema mchana radio one imetangaza kwamba watu walio katika majengo marefu wanapashwa kutoka katika majengo hayo kwa usalama wao.Shule ya msingi Kibonde maji watoto wamesambaratika na wazazi wanaohaha kusaka watoto wao wamekuwa hawajui nini cha kufanya.Mmoja wa madereva wa Mbagala aliyejitambulisha baba halima amesema alilazimika kukimbilia Mkuranga kwa hofu jinsi mitikisiko ilivyokuwa inamchanganya pale Mbagala rangi tatu.

SHEREHE ZA MUUNGANO LONDON

Mheshimiwa Balozi, akiwa na Maofisa wengine wa Ubalozi, baada ya kumalizika kwa Ibada ya kuiombea Nchi yetu Tanzania.
Ibada hiyo uandaliwa kila Mwaka na Kanisa la Westminister Abbey inapofika siku ya Muungano. Kanisa la Westminister Abbey huandaa Ibada kwa Kila Nchi Mwanachama wa Commonwealth zinapofika siku za nchi zao Mataifa yao. Kulia mwa picha ni Bwana David Nginilla, Bwana Amos Msanjila, Mh. Balozi, Mama Mwanaidi. S. Maajar, Dada Caroline Chipeta, na Bwana Clement Kiondo.
Mheshimiwa Balozi, Mama Mwanaidi S. Maajar {Pili Kushoto}, akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na Wawakilishi wa Jumuiya za Watanzania kwenye Sherehe za kuadhimisha Miaka 45 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Toka kulia mwa picha ni Mh. Abubakar Faraji, Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania hapa Uingereza, Bwana Katega-Muwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania Birmingham, Bwana Maina- Mwenyekiti wa CCM Reading, Bwana Jackson- Mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania Birmingham, na Bwana Fredy {nyuma ya picha}- Mtanzania na Mtangazaji kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC-London

RISASI LEO


KESI YA ZOMBE

MSHITAKIWA wa 12 katika kesi inayomkabili aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Abdallah Zombe na wenzake wanane, Bakari Rajab, ameeleza alivyoshuhudia mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini na dereva mmoja katika msitu wa Pande, Dar es Salaam.
Mbele ya Jaji wa Mahakama ya Rufani, Salim Massati, jana Rajab alidai kuwa alishuhudia askari mwenzake Koplo Saad akimpiga risasi mmoja wa watuhumiwa Januari 14, 2006. ZAIDI....

Tuesday, April 28, 2009

MISS AFRIQUE 2009

LADIES AND GENTLEMEN,BEHOLD YOUR BREATH AND AWAIT THE FIRST OF THIS KIND OF BEAUTY CONTEST DABBED MISS AFRIQUE 2009.THIS WHOLE NEW EVENT IS BROUGHT TO YOU BY THE INTERNATIONAL FASHION DESIGNER AND THE MAIN BRAIN BEHIND JULIE MODELS INTERNATIONAL MISS JULIE.AS OPPOSED TO TODAY'S BEAUTY PAGEANTS THATS ARE USUALLY PORTRAYED IN THE MEDIA,THIS ONE IS GOING TO BE QUITE UNIQUE BECAUSE OUR PURPOSE IS GOING TO BE FOCUSED ON BEAUTY WITHIN WHERE BY WE GOING TO HAVE AN ARRAY OF DIFFERENT GIRLS OF ALL SHAPES AND SIZES.SINCE THIS IS GOING TO BE SOMETHING QUITE NEW AND INTERESTING ,AM SURE YOU CANT AFFORD TO MISS IT.PLEASE MAKE YOUR ADVANCE TICKET BOOKINGS BY DIALING THE NUMBERS BELOW.

JULIE-07940072901 OR FOR MORE INFO JOIN FACEBOOK JULIES MODELS.


KHANGA NA VITENGE


Vivazi vilivyoundwa kwa kutumia vitambaa vya vitenge na Kanga vimechukua nafasi kubwa katika anga la mitindo si Bongo pekee kwani hata nchi za wenzetu tumeshuhudia hilo.Madezigner wengi wa hao wa nyumbani wamejikita katika matumizi ya kanga na kama hawatotumia kwa vazi lolote, basi vazi litanakshiwa kwa kanga au kitenge.Nimeweza kushuhudia kwa wabunifu kama Mustafa Hassanali,Asia Idarus,Khadija Mwanamboka, Robby , Fatma Amour na wengineo wengi.Nilimshuhudia pia mwanamuziki wa Marekani Estella akiwa wametinga vazi lililoshonwa kwa Kanga, hakika inavutia.Siku za karibuni wabunifu watanzania kupitia mitindo House walifnya onesho la mavazi nakulipa jina la Kimaso maso ambapo walikuwa na nia ya kuonyesha mavazi ya maharusi wenye asili ya kiafrika mwisho wasiku walijikuta wengi wakiwa wametumia kanga na vitenge kama nakshi ya mavazo hayo.Habari ndo iyooo kama nawe ni mteja wa Fashion jitahidi uwe na kamshono ka kanga kama si kitenge shost.




MENGI ASHAMBULIWA

MAWAZIRI wawili, Sophia Simba na George Mkuchika jana walimshambulia mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi ambaye wiki iliyopita alitangaza majina ya wafanyabiashara watano wenye asili ya Kiasia, akisema ni mafisadi waliokubuhu.
Simba, ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na Mkuchika, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo walisema mfanyabiashara huyo wa jijini Dar es salaam "amechemsha".
Mengi alitangaza majina ya wafanyabiashara hao Alhamisi iliyopita akisema ni kati ya watu wasiozidi 10 ambao alidai wanaifilisi nchi na kutaka wadhibitiwe mapema kabla hawajaitingisha na kuiyumbisha nchi.
Hata hivyo, Mengi, ambaye alidai katika taarifa yake kuwa juhudi za Rais Jakaya Kikwete zinakwamishwa na watu hao, hakueleza jinsi watano hao wanavyoitafuna nchi zaidi ya kusema kuwa wanatorosha fedha wanazozipata 'kifisadi'.
Jana, kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam mawaziri hao wawili walitoa kauli za kumshambulia mwenyekiti huyo mtendaji wa makampuni ya IPP, kauli ambazo zinadokeza mtazamo wa serikali katika mjadala unaoendelea wa vita dhidi ya ufisadi na vinara wake.
Waziri Simba, ambaye wizara yake pia inawajibika katika vita dhidi ya ufisadi, alisema: "Kakosea... watoto wa mjini wanasema kachemsha."
Simba alitoa msimamo huo jijini Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya kufungua semina ya wadau wa vyama vya siasa kuhusu namna ya kuiboresha Sheria ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995.
Simba alisema Mengi hana mamlaka hayo ya kutaja watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.
Kabla ya kujibu swali kuhusu kitendo cha Mengi, ambaye anamiliki televisheni ya ITV na kituo cha redio cha Radio One Stereo, kutaja majina ya watu hao aliowaita mafisadi papa, Simba alihoji: " Hapa kuna mtu wa ITV?."
Baadaye alisema: "Sikilizeni, kwanza kitendo alichokifanya Mengi si sahihi, kakosea hawezi kuhukumu watu, mamlaka hayo anatoa wapi?"
Simba, huku akionekana kama mtu ambaye alikuwa akitafuta jukwaa kuzungumzia suala hilo, alisema Mengi amekosea kwa kuwa baadhi ya watu aliowataja wana kesi mahakamani.
"Anahukumu watu," alisema. "Kuna mtu kama Jeetu (Patel) ana kesi mahakamani (EPA), sasa unapokuja kusema ni fisadi wakati mahakama haijathibitisha, unakuwa na maana gani.
"Kwanza kwanini awatuhumu wafanyabiashara wenzake tu, ina maana si ana nia mbaya nao."
Alisema Mengi amechukua uamuzi huo kama vile serikali, wakati serikali ipo siku zote na imekuwa ikifanya kazi zake kwa umakini kwa kufuata misingi ya sheria.
"Serikali ipo na inafanya kazi kwa misingi ya sheria, sasa yeye kukaa na kutangaza watu nasema si sahihi kabisa. Mahakama pekee ndiyo inaweza kumtia mtu hatiani, lakini huwezi kuhukumu watu kama hakuna mamlaka."
Waziri Simba, ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), alisema Mengi hapaswi kutumia vyombo vyake vibaya.
"Asitumie vyombo vyake kufanya atakavyo yeye. Huwezi kukaa katika chombo chako na kuanza kuhukumu watu. Kila mtu akifanya hivyo itakuaje," alihoji.
Akiongea na Mwananchi baada ya kupata taarifa za kauli ya Simba, Mengi alisema: "Namuombea kwa Mwenyezi Mungu na kwa maskini wa Tanzania ili wamsamehe kwa sababu hajui anenalo."
Mengi hakutaka kuzungumza zaidi kuhusu hatua hiyo ya Mama Simba.
Naye Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali itamchukulia hatua za kisheria Mengi iwapo itabainika alikiuka taratibu na kanuni za nchi kwa kutangaza majina ya watu anaowatuhumu kwa ufisadi.
Mkuchika alisema jijini Dar es Salaam jana kwa sasa serikali inafanya uchunguzi juu ya suala hilo na itatumia mikanda ya video pamoja na maelezo ya kimaandishi aliyoyatoa Mengi siku alipokutana na waandishi wa habari.
"Tumekusudia kupata ule mkanda wa video, pia tusome maelezo yake ya kimaandishi... tukigundua kuna mahala ambapo sheria haikuzingatiwa, (Mengi) atachukuliwa hatua," alisema Mkuchika.
Mkuchika alisema serikali imepokea malalamiko mengi kutoka kwa watu wengi, wakishutumu hatua iliyochukuliwa na Mengi, ambaye pia anamiliki viwanda vya vinywaji.
Bila kutaka kuwataja majina, Mkuchika alisema miongoni mwa walalamikaji, wapo walioeleza kuwa vyombo vya habari vya mfanyabiashara huyo havikuwatendea haki watuhumiwa waliotajwa kuwa ni mafisadi wakuu

POZI !!!








KATUNI YA LEO


CELEBS IN MONACO

Folks are playing some poker over in Monaco. Christina Milian and her man Dream kicked it with Nelly at the Monaco Celebrity Poker Tournament:

SANAA .............................................

Actress Sanaa Lathan was spotted in Manhattan last night after leaving dinner at the popular Da Silvano. Isn’t she so beautiful and classy?! A few journalists have tried to convince me that she’s a total b*tch in person but I wasn’t trying to hear it. Oh, and that’s Kim K in the back channeling Beyonce.

MUNGU AKUWEKE MAHALA PEMA PEPONI ASHA SAPI MKWAWA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana alienda kuwafariji ndugu na jamaa wa Marehemu bibi Asha Adam Sapi Mkwawa wakati Rais alipokwenda kuwapa pole kufuatia kifo cha mke huyo wa spika wa Zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Monday, April 27, 2009

YNONNE CHAKACHAKA ABUBUJIKWA MACHOZI MTWARA

MWANAMUZIKI wa Afrika Kusini, Yvonne Chakachaka ijumaa iliopita alibubujikwa na machozi baada ya kusikia kuwa mtoto aliyekuwa amelazwa kwa malaria amefariki dunia na mama yake kuondoka na maiti mgongoni.

Yvonne ambaye pia ni Balozi wa Malaria duniani alikuwa akigawa vyandarua vyenye dawa katika wodi namba tano ya hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Lugula alipokuwa amelazwa mtoto huyo.
Alipofika wodini hapo, aliambiwa kuwa alikuwapo mgonjwa huyo, lakini alifariki dunia jana na mama yake akalazimika kuubeba mwili wa marehemu mgongoni kutokana na kukosa usafiri, ndipo mwanamuziki huyo alishindwa kuzuia machozi.
“Najua wengi mmeshangaa nilivyolia, lakini kama mzazi imeniuma, kwa kuwa siamini kama kunaweza kuwa na tukio kama hilo katika bara letu la Afrika,” alisema.

Alisema hiyo ilikuwa siku mbaya maishani kwake na hawezi kuondokana na kumbukumbu ya tukio hilo.
“Nimeamua kununua gari moja ambalo litakuwa linatumika maalum kwa ajili ya kina mama na watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa huu sugu hapa nchini.”

Alisema kuwa kwa sasa anaangalia uwezekano wa kuja kuishi nchini na kama ikiwezekana iwe Mtwara, ili aweze kusaidiana na akinamama ambao wanapata matatizo ya watoto na uzazi. “Sioni sababu ya sehemu kama hii nzuri kuwa na matatizo, mimi nimeipenda Mtwara, nimetembelea baadhi ya mikoa Tanzania, lakini naona nchi hii ni ya kuwa makazi yangu ya baadaye,” alisema.

Chakachaka ambaye aliwasiri wiki iliopita kwa ajili ya kushuhudia maadhimisho ya siku ya Malaria duniani alitembelea Hospitali ya Ligula na baadaye kufanya onyesho katika viwanja vya mashujaa na kuhutubia wananchi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyekuwa mgeni rasmi, alisema kuwa mikoa ya kanda ya ziwa ndio imekuwa ikiongoza nchini kwa kuwa na asilimia 34 ya maambukizo ya malaria ikifuatiwa na mikoa ya kusini asilimia 30 na mikoa ya magharibi asilimia 21 wakati mikoa mingine ni asilimia 14.

MIAKA 45 YA MUUNGANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jakaya Kikwete akikagua gwaride wakati wa maadhimisho ya miaka 45 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Dar es Salaam jana.

Saturday, April 25, 2009

POZI !!!


Miss Tanzania no 2 mwaka 2008 Slivia Mashuda (aliyekaa) akiwa na Laila Bhanji.

MH.PHARES KABUYE AFARIKI KATIKA AJALI YA BASI


MBUNGE wa Jimbo la Biharamulo Magharibi mkoani Kagera Bw. Phares Kabuye amefariki kwa ajali ya basi akiwa safarini kutoka Kagera kwenda Dar es Salaam kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tanzania Labour Party (TLP) uliopangwa kufanyika kesho.Katika Mkutano huo, Bw. Kabuye alikuwa ameomba kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho kwenye uchaguzi huo, uliosubiriwa kwa shauku na wanachama wengi wa chama hicho.

Marehemu Kabuye, Mbunge aliyesimamishwa wa TLP, alifariki jana saa mbili asubuhi eneo la Magubike, wilayani Kilosa, Morogoro. Katika ajali hiyo, watu wengine wawili walikufa na wengine 54, kujeruhiwa.Ajali hiyo ilihusisha basi la RS Investment, lenye namba za usajili T934 ABK lililoserereka na kupinduka likiwa kwenye mwendo.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Samuel Sitta amethibitisha tukio hilo na kueleza kusikitishwa kwake na kifo cha Mbunge huyo ambaye hadi mauti yakimfika , alikuwa akipigania rufani yake mahakamani kupinga kuvuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Kagera .

Abiria walionusurika, walisema basi hilo liliserereka na kupinduka baada ya mtu aliyekuwa akiendesha anayedaiwa kuwa utingo, kushindwa kulimudu.Walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa basi hilo lilikuwa katika mwendo na waliokaa sehemu ya mbele, walisikia dereva aliyekaa pembeni akimwelekeza utingo huyo kushika breki haraka.Kufumba na kufumbua, basi hilo lilihamia upande wa pili wa barabara na kupinduka tairi zikiwa juu na kugeuka lilikotoka. Dereva na utingo huyo walikimbia baada ya ajali hiyo na hawajulikani waliko.

HARUSI YAPIGA HODI KWA MANGE KIMAMBI

Lance akiwa amepiga magoti mara baada ya kukubaliwa uchumba wa ndoa na kumvisha pete Mange Jana jioni Kempsiki Hotel.
Kutoka shoto Basila Mwanukuzi, Mange na K-lynn

Mange (pili kulia) katika Pozi na mumewe mtalajiwa (kulia) na marafiki zao katika hafla fupi iliofanyika jioni ya jana Kempsiki Hotel jijini Dsm.


MWANAMICHEZO BORA 2008


Meneja uhusiano wa benki ya Standard Chatered Hoyce Temu na afisa mwanadamizi wa uhusiano wa benki ya NMB Shayrose Banji wakiteta jambo na Irene Kiwia katika sherehe za kumtangaza mchezaji bora wa mwaka 2008 zilizofanyika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski jana sherehe hizo zilizoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA.

Friday, April 24, 2009

MENGI AMWAGA UPUPU



Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, amewataja watu watano wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi mkubwa nchini na kuitaka serikali iwashughulikie haraka iwezekanavyo ili kuinusuru nchi kuyumbishwa nao. Watu hao, ambao Mengi alisema kwamba wanatuhumiwa kuwa ni `mafisadi papa`, ni pamoja na Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM) na Halmashauri Kuu ya Chama hicho (NEC-CCM) Taifa, Rostam Aziz. Aliwataja wengine, kuwa ni wafanyabiashara, Tanil Somaiya, Yusuf Manji, Jeetu Patel na Subash Patel, ambao alisema wanatuhumiwa kuiba mabilioni ya wananchi na kuzihamishia nje ya nchi. ``Hawa wanatuhumiwa kuiba mabilioni ya fedha za wananchi, na baya zaidi fedha hizo zimehamishiwa nje ya nchi,`` alisema Mengi alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za IPP Limited, jijini Dar es Salaam jana na kuongeza: ``…mafisadi wote na hasa wale wanaotuhumiwa kuwa mafisadi papa ni lazima washughulikiwe, la sivyo wataiyumbisha na kuitingisha nchi yetu. Ni lazima Watanzania tuone kwamba sasa tumefika mahali pa kusema imetosha.``

LIL KIM ASHINDANA NA MICHAEL JACKSON KULA VISU MWILINI

PICHA ZA ZAMANIPICHA ZA SASA

WANJA LA KIMATAIFA LAJA !!!


Baada ya hadithi za miaka teleee...hatimaye serikali la Mh. Raisi JK.....liko kwenye mchakato wa ukweli kwa ajili ya ujenzi wa wanja kubwa kabisa la kisasa la midege (EYAPOTI) kitakachokidhi mahitaji ya usafiri wa anga katika miaka 50 ijayo. Taarifa iliyotufikia imedai kuwa mpaka sasa serikali imebaini sehemu 2...maeneo ya Mkoa wa Pwani ambayo yanaweza kujengwa kiwanja hicho kitakachokidhi mahitaji . Kwa mujibu wa taarifa kutoka wizara ya Miundombinu,maeneo hayo yako Bagamoyo na Mkuranga ambapo taratibu za kuyapima na kupata hati zinafanywa na wizara hiyo, kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege. Sambamba na hatua hiyo serikali inao mpango wa muda mrefu wa kuendeleza Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere ambapo hivi sasa inakamilisha mazungumzo na Kampuni ya kimataifa kutoka China ya China Sonangol kwa ajili ya kupanua na kuendeleza kiwanja hicho.

Kazi ya usanifu na upanuzi wa kumbi za kuondokea na kufikia wageni katika uwanja huo ilikuwa imeshaanza na inafanywa na Mhandisi kutoka Kampuni ya Aeroproject hapa Town na inatarajiwa kukamilika mwezi huu.

BSS BONGO KUFANYIKA KESHO NA KESHOKUTWA

Mkurugenzi wa Benchmark waandaaji wa Bongo Star Seach Ritah Paulsen akizungumza na wanahabari katika mako makuu ya Vodacom jengo la PPF Tower wakati alipoongea na wanahabari kuelezea juu ya shindano la BSS linalotarajiwa kufanyika jumamosi na jumapili mkoani Dar es alaam kulia ni Nector Foya meneja mawasiliano Vodacom


Shindano la kutafuta wawakilishi wa mkoa wa Dar es alaam katika shindano la BSS 2009 litafanyika kuanzia jumamosi mpaka jumapili wiki hii katika ukumbi wa New World Cinema ambapo zaidi ya washiriki wapatao 2000 wanatarajia kujitokeza ambapo mshindi wa mwaka huu anatarajiwa kuondoka na zaidi ya milioni 15 ambazo mshindi wa mwaka jana alijishindia.Kampuni ya simu za mkononi Vodacom ni wadhamini wa shindano hilo linaloratibiwa na kampuni ya Benchmark Production ambapo zaidi ya vijana 8000 wameshiriki katika mchujo huo mikoani kote ambako shindano hilo limefanyika na vijana 35 wameingia raundi ya pili .

GAZETI LA IJUMAA LEO


Thursday, April 23, 2009

HAYA WAZAIRE WAJITOKEZE TUONE ???


KATUNI YA LEO


KAZI IPO !!!!!!!!

Mgonjwa: Daktari naumwa sana moyo.

Daktari: Wewe ni mpenzi wa timu gani ya mpira wa miguu?

Mgonjwa: Kwa Tanzania mimi ni shabiki wa Simba na Ulaya mimi ni mpenzi wa Manchester United.

Daktari: Na unafanya kazi wapi?

Mgonjwa: Nilikuwa nafanya kampuni ya GTV, baada ya kufa nikapata kazi Paradise Hotel Bagamoyo.

Daktari: Una akiba yoyote ya fedha benki?

Mgonjwa: Ndiyo, akiba yangu yote ya fedha ipo DECI.

Daktari: Mmmh, unaishi wapi?

Mgonjwa: Naishi Kwembe wilayani Kinondoni.

Daktari: Duh, subiri kufa maana hakuna tiba mbadala ya maradhi yako.

MM.KIKWETE NCHINI MAREKANI

Mama Salma Kikwete akiwa na Mke wa Waziri Mkuu wa UK Sarah Brown ktk mkutano wa wake za marais huko USA.

MAIMARTHA ATUNIKIWA TUZO

Mtangazaji wa kituo cha Luninga cha East Africa cha Jijini Dar es Salaam, Maimartha Jesse amepewa tuzo ya Mtangazaji Bora kwa kipindi cha mwaka 2008 mpaka 2009 na kampuni ya mitindo ya Smilling Faces baada ya kufanya vyema katika taaluma hiyo na kupigiwa kura nyingi kupitia kampuni hiyo.

RIHANNA IS LIVING WITH CHRIS BROWN

The 'Umbrella' singer and her 19-year-old on/off boyfriend - who has pleaded not guilty to assaulting her - are said to have rekindled their relationship, but are doing all they can to keep out of the spotlight.
A friend of Rihanna's told the Chicago Sun Times newspaper: "They have spent quite a few nights together. Unfortunately, Rihanna still wants him and has said to us all, 'Get over yourselves. I'm with him, so deal with it.' She has told us she won't be going public with the relationship for a while."
Rihanna wants strong women to join her. This is a 'women empowerment' type of tour.
Chris is accused of hitting, biting and choking Rihanna until she was unconscious in his car on February 8.
He has been charged with felony assault and making criminal threats, and faces over four years in prison if convicted.
Although the pair briefly reunited after the incident, they have since been taking time apart from each other to consider their future.
Earlier this week, it was claimed Rihanna was dating Los Angeles Lakers' star Andrew Bynum after the pair were spotted enjoying an intimate dinner together.
However, Andrew has since denied the claims, insisting the pair are simply close friends.

NANNY TO CARE FOR MERCY

Madonna has left a nanny to care for the Malawian child she is attempting to adopt.
The 50-year-old singer - who failed in her initial bid to raise four-year-old Mercy James because she hadn't met the requirements of living in the African country for 18 months - has instructed members of her staff to look after the tot at Kumbali Lodge, where the star stayed during her visit earlier this month.
A source said: "During her farewell party at the lodge, Madonna instructed a nurse and a nanny to remain behind and care for Mercy while her lawyers appeal."
However, Judge Esme Chombo thinks Mercy should return to her orphanage 250 miles away, but that suggestion has been met with criticism from Mercy's guardian and extended family.
During her farewell party at the lodge, Madonna instructed a nurse and a nanny to remain behind and care for Mercy while her lawyers appeal.
Orphanage director Anne Chikhwaza said: "As Mercy's legal guardian I authorise where she goes. She is staying with Madonna's people as a visitor. There is nothing wrong with that."
Mercy's uncle Peter Baneti also said the family wanted Madonna to take care of Mercy immediately.
He said: "We don't agree with the judge's decision to reject Madonna's intention to adopt Mercy. As a family we consented to the adoption."
Earlier this week, it was revealed Madonna's adoption appeal date had been set for May 4 and her case will be heard by three judges at Malawi's Supreme Court of Appeal.