.

.

.

.

Wednesday, May 13, 2009

TWANGA PEPETA YAJA NA ALBAMU MPYA

BENDI ya African Stars "wana Twanga Pepeta" itazindua albamu yake ya 10 Juni 5 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania, ASET, Asha Baraka alisema albamu yao mpya inajulikana kwa jina la MWANA DARESSALAAM , wimbo ambao umetungwa na Charles Gabriel maarufu kwa jina la Charles Baba.Baraka alisema kuwa hawakuweza kuzindua albamu mwaka jana kutokana na kuipa nafasi alabamu yao ya Mtaa wa Kwanza kuingia zaidi sokoni na mwaka huu wameona ni muafaka kuzindua albamu mpya ili kuendelea kutoa burudani kwa wapenzi wake.
Kwa mujibu wa Baraka, baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ni Sumu ya Mapenzi, Shida ni Darasa, Sitaki Tena Kupenda na Utambulisho wa Ubaya ambao umetungwa na Saulo Furguson.Nyimbo nyingine ni Nazi Haivunji Jiwe na Rafiki Mbaya. Alisema kuwa bendi yake kwa sasa inajifua vilivyo ili kutoa burudani safi siku hiyo ya uzinduzi.

No comments:

Post a Comment