.

.

.

.

Saturday, June 25, 2011

SHAA KUTUMBUIZA KESHO BBA


Mwanamuziki wa kike kutoka Tanzania ambaye aliwahi kuwa ndani ya kundi la wakilisha na kupata zawadi ya kutembelea jiji la Johannesburg akiwa kama Coc Cola Popstar, kesho atakuwa ni mtumbuizaji katika shoo ya kutoka kwa mmoja kati ya washiriki waliomo katikia shindano la Big Brother Amplified.

Shaa anaenda huku washirikii wote wawili wa kitanzania wakiwa wamwtoka katika shindano hilo ingawa anategemea kupokelewa kwa shangwe na mashabiki wake wa kitanzania waishio katika jiji hilo ambapo pia atahudhuria sherehe maalum ya BigBrother baada ya washiriki husika kutolewa.

Huyu atakuwa ni mwanamuziki wa pili anayesimamiwa na kampuni ya Unity Entertainment kwenda kutumbuiza katika shindano hilo ambapo kwa mujibu wa kumbukumbu zetu ni kwamba Ambwene yesaya pia aliwahi kuwa mmoja wa watumbuizaji kutoka tanzania ambao waliwahi kufanya onesho katika sherehe za za BigBrother.

Walio katika hatari ya kutoka wiki hii ambao ndio watakaosindikizwa na shaa ni pamoja na Wendal, Sharon, Zeus, Hanni, Vimbai, Felicia na Milicent.

hawa wote ni kutoka katika jumba zima la Heads na aliyesalimika humu ni Vina tu ambaye hajatajwa kuingia katika msukosuko wa kutoka.

No comments:

Post a Comment