.

.

.

.

Monday, August 31, 2009

KATUNI YA LEO




ZITTO AJITOA

Mbunge wa kigoma Kaskazini na katibu mkuu wa chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) Zitto Kabwe amejitoa kugombea uenyekiti wa chama hicho ili kulinda mshikamano na umoja ndani ya Chadema na kutekeleza busara za wazee wa chama hicho.
Habari zinasema Zitto Kabwe ameamua kuacha kugombea kutokana na vikao mbalimbali vya wazee wa chama hicho vilivyokaa na kumsihi asigombee ili kutokigawa chama hicho katika kipindi hiki ambacho uchaguzi mkuu unakaribia ili kutokigawa chama na kuendeleza mshikamano katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2010.
Zittio Kabwe hivi karibuni alitangaza kugombea uenyekiti wa chama hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, baada ya kutangaza nia yake hiyo kulitokea malumbano mengi katika vyombo mbalimbali vya habari kitu ambacho huenda kimepelekea wazee wa chama hicho kukaa na kumshauri Mb. Zitto kutogombea nafasi hiyo ili kulinda maslahi ya chama, mshikamano na umoja ndani ya chama hicho.

KIBOKO YA HA-SHE- EM

Baraka (Kulia) ambaye ndiye mtu mrefu kuliko wote Tanzania akiwa katika pozi na mchezaji Hasheem Thabit (watatu shoto) ambaye anachezea ligi ya NBA nchini Marekani.Huenda Baraka naye siku za mbeleni akafikia alipo Hasheem kwani anafuliwa hivi sasa na kocha Bahati (pili Kulia)

Saturday, August 29, 2009

FREEMAN MBOWE KUNUSULIWA NA ZITTO KABWE

KATIKA kile kinachoelezwa kuwa ni kunusuru mustakabali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wazee wa chama hicho leo wanakutana, huku taarifa zikieleza kuwa Zitto Kabwe, ambaye ametangaza kumvaa Freeman Mbowe katika kinyang'anyiro cha Uenyekiti Taifa, anaandaliwa nafasi ya ukatibu mkuu kunusuru mpasuko ndani ya chama hicho.
Mkutano huo unaowahusisha waasisi wa Chadema, akiwamo wenyekiti waliopita, Edwin Mtei na Bob Makani pamoja na wazee wengine kadhaa, unafanyika katika kipindi ambacho tayari wadadisi wa masuala ya siasa wameonyesha wasiwasi wa chama hicho kupasuka iwapo hakutakuwa na busara ya kufanya maamuzi sahihi katika mchakato huo wa uchaguzi.
Iwapo ajenda hiyo ya kumpa Zitto nafasi ya katibu mkuu, itajadiliwa na kupitishwa leo, moja kwa moja itakuwa ni kwa ajili ya kumnusuru Mbowe na chama katika hatari ya kugawanyika. Juzi wazee hao, kwa nyakati tofauti, waliliambia gazeti hili kwamba, uamuzi wa Zitto kugombea ni ukuaji wa demokrasia ndani ya chama hicho.
Mzee Mtei alisema "ndiyo maana kinaitwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo", huku mzee Makani akisema "hakuna mpasuko kwani ni lazima kutakuwa na watu wanaomuunga mkono Zitto na Mbowe, hivyo huo si mpasuko".
Lakini Mwananchi ilipata habari jana jioni zikisema katika kupiga hatua moja mbele kunusuru chama hicho, wazee hao wamepata wazo jipya ambalo ni kufikiria namna bora ya kumtuliza Zitto kwa kumpatia nafasi hiyo ya mtendaji mkuu wa chama ambayo sasa inashikiliwa na Dk Willibrod Slaa, mmoja wa viongozi shupavu ambao wanaheshimika sana katika chama hicho kiutendaji.
Hata hivyo, bado swali linabaki kwamba iwapo Zitto atapewa nafasi hiyo, Dk Slaa atakuwa na nafasi gani kwenye chama hicho.
Tangu kuanza kwa maandalizi ya uchaguzi, Dk Slaa alishawishiwa na wanachama agombee nafasi ya makamu mwenyekiti, lakini alikataa kwa madai anataka kupumzika kazi za chama.
Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya uongozi ndani ya chama hicho wanasema kuwa kuna kundi la wanachama ambao wanataka Dk Slaa agombee urais 2010, lakini mara kadhaa yeye amekuwa akidai hataki nafasi hiyo na kwamba ataendelea kuwatumikia watu wa Karatu kwa nafasi ya ubunge.
Kwa upande wa Mbowe, hali inaonyesha kwamba safari hii hatagombea urais na badala yake ataenda Hai kwa ajili ya kugombea ubunge.
Ingawa watu wengi wanadhani Zitto amekurupuka kugombea nafasi hiyo, lakini watu ambao walio karibu na mwanasiasa huyo wanadai kuwa amejenga mtandao mkubwa kwa muda mrefu ambao utamsaidia sana kupambana na Mbowe.
"Zitto ameshiriki sana kuweka vijana hasa mikoani na Mbowe anakubalika na watu wa mjini na hasa Dar es Salaam na Kilimanjaro, lakini Zitto amejijenga," alisema mmoja wa watu walio karibu na Zitto, 33.
Mapema jana kabla ya taarifa hizo mpya, Zitto, akiwa jijini Dar es Salaam, alisema atakuwa tayari kupokea ushauri wowote utakaotolewa na wazee wa chama hicho.
Alifafanua kuwa huu ni wakati wa uchaguzi, lakini baada ya hapo Chadema itapaswa kuwa chama kimoja kisichokuwa na kambi yoyote.
Zitto alisema kwa mantiki hiyo iwapo atashinda, bado atapaswa kushirikiana na Mbowe na akishindwa, Mbowe atapaswa kushirikiana naye (Zitto), hivyo wanaoeneza propaganda chafu, hawajui nini chama hicho kinapaswa kutendewa.
Zitto, ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, pia alionyesha kuchukizwa na kile kinachoelezwa kwamba anatumiwa na mafisadi na kuhoji: "Ni akina nani hao wanaonitumia... wananitumia ili iweje?"
"Mimi Chadema ni basi langu ambalo nasafiria au sawa na mtumbwi wangu baharini, sasa nitawezaje kuivuruga, halafu nitapata faida gani au nitakwenda wapi,"alihoji.
Alisema kamwe hawezi kutumiwa na mtu yeyote kuvuruga chama hicho kwani ndilo tegemeo la Watanzania kama chama mbadala cha kushika dola.
Zitto hakusita kuweka bayana kwamba Chadema pia ina safari ndefu ya kuunganisha vyama vya upinzani na kujenga umoja imara ambao utakuwa na lengo moja tu la kuleta mageuzi.
"Ukweli ni kwamba NCCR, CUF, TLP na vyama vingine vya upinzani vinatuhitaji na sisi lazima tunavihitaji kushirikiana navyo kwenye maeneo mengi, sasa nitawezaje kuua Chadema badala ya kuimarisha na kuunganisha na wengine," alihoji.
Zitto, mwenye umri wa miaka 33 na mmoja wa wabunge ambao wamekuwa wapambanaji wakubwa ndani ya Bunge, alisema yeye bado mwanasiasa kijana kuliko wote kwenye nafasi ya juu ya uongozi wa Chadema, hivyo haiingii akilini kwamba ataweza kuvuruga chama wakati bado ana malengo ya baadaye kisiasa.
Aliongeza kusema: "Kwa sasa wakati tunajipanga kuelekea katika uchaguzi, mimi nadhani inatupasa tuangalie zaidi maslahi ya chama. Bado kuna maisha baada ya uchaguzi, isije kuwa baada ya uchaguzi tukashindwa kuangaliana. Kama nikishinda nitakuwa katika nafasi nzuri ya kumpigia kampeni Mbowe huko Hai nikiwa kama mwenyekiti wake katika uchaguzi mkuu ujao," alisema Zitto.
Zitto alifafanua kwamba alilazimika kujaza fomu za kugombea kiti hicho akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere baada ya kushauriwa sana na wenyeviti mbalimbali wa mikoa wa chama hicho.
"Kuna watu wanasema nilijaza fomu kwa mtindo wa kakakuona, lakini inatakiwa wajue kuwa siasa ni staili. Mimi binafsi sikutaka kugombea uenyekiti, lakini shinikizo la wanachama ndilo lililo lilinifanya nigombee, nilijaza fomu nikiwa uwanja wa ndege wakati nikielekea Ujerumani baada ya kuona siwezi kuendelea kuyakataa maombi ya wanachama," alisema Zitto.
"Mimi sina ugomvi wowote na Mbowe labda yeye lakini, kesho wazee wa chama chetu tutakutana nao ili kuangalia kama kuna tofauti zozote tuzimalize," alisema Zitto.
Zitto alisema ana uwezo wa kukiendesha chama kutokana na kuwa na uzoefu mkubwa katika siasa za kitaifa na kimataifa.
"Mimi nimekuwa mshauri wa rais wa Ujerumani kuhusu mambo ya kiuchumi wa bara la Afrika kuanzia mwaka 2006, ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali yenye mashirika zaidi ya 193 na thamani ya zaidi ya Sh 3 trilioni, nitashidwa kuiongoza Chadema," alihoji Zitto.
Hata hivyo, alisema kama atashinda na kukishika kiti hicho mwenyekiti wa sasa, wa chama hicho Mbowe atakuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho kama katiba yao inavyosema.
Naye Mbowe alisema propaganda dhidi ya chama hicho haziwezi kukiyumbisha.
Mbowe, ambaye atagombea nafasi kwa mara ya pili, alisema chama hicho kimetoka mbali na kimejengeka katika misingi ya kidemokrasia, hivyo kila jambo linafanywa kwa uwazi na kwa kufuata kanuni na taratibu za chama hicho.
Mbowe aliliambia gazeti hili jana kuwa mamluki hawakosekani katika taasisi yoyote ile na kusisitiza kuwa maamuzi yote yanafanywa na vikao ndani ya chama na hakuna hata kikao ambacho kimeshakaa hadi hivi sasa.
"Propaganda kutoka kwa watu wa nje na hata baadhi ya vyombo vya habari haziwezi kuvuruga chama chetu, ni wazi kuwa mamluki hawakosekani katika taasisi yoyote ile, lakini chama chetu kina utaratibu wa kuamua mambo yake kupitia vikao mbalimbali. Hakuna maamuzi yanayotolewa bila kuafikiwa na vikao," alisema Mbowe.
Mbowe alisisitiza kuwa uamuzi wa Zitto ni matokeo ya demokrasia ndani ya chama na kuongeza kuwa ana imani kuwa chama kitapita katika kipindi ambacho ni kigumu katika siasa za demokrasia.
"Nina imani tutavuka salama; ni vema Watanzania wakaangalia chama si kwa utashi wa mtu anayeongoza bali kwa kile wananchi wanachofanyiwa na chama. Hiki ni chama cha Watanzania na tuna imani tutavuka salama," aliongeza Mbowe.
Aliongeza hata baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao, hatarajii kuwa kutakuwa na chuki na kutoelewana kwa viongozi wa chama hicho kwani wote wanafanya kazi kwa kujitolea na hakuna mshahara wanaolipwa.
"Viongozi wote wa ngazi za juu wanafanya kazi kwa kujitolea, tunachotafuta ni kazi ya kujitolea kuwatumikia wananchi na hakuna 'ulaji'…hakuna anayelipwa mshahara," alifafanua Mbowe.
Mwananchi ilipotaka kujua kama atagombea urais kwa tiketi ya Chadema iwapo atabaki kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Mbowe alisema: "Nafasi ya kugombea urais si wajibu wa kudumu wa mwenyekiti. Ni chama ndicho kitakachopendekeza nani na kwa sifa zipi ndio anafaa kugombea nafasi hiyo, alisema.
Mkutano mkuu wa Chadema umepangwa kufanyika Septembe 3 na 4 ambapo utatanguliwa na mkutano wa kamati kuu Septemba 30, na mkutano mkuu wa kwanza wa baraza la wazee utafanyika Septemba 31 mwaka huu.
Mwisho.
Hata hivyo, hadi sasa chama hicho kipo kwenye kipindi cha kigumu cha mpito kuelekea kwenye uchaguzi huo ambao ni mtihaani wa pili baada ya ule wa kifo cha Makamu Mwenyekiti Chacha Wangwe.

Habari hii imeandaliwa na Ramadhan Semtawa, Claud Mshana na Fred Azzah

RISASI JUMAMOSI


Friday, August 28, 2009

MIAKA 45 YA JWTZ


Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje Ulinzi na Usalama Wilison Masilingi mara baada ya ufunguzi wa maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45. Mh. Masilingi alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Maadhimisho hayo yanayoendelea katika kikosi cha 603 cha jeshi eneo la Airwing ,Ukonga jijini Dar es salaam.Wa kwanza Kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein mwinyi ambaye aliambatana na Naibu wake Dkt. Emannuel Nchimbi (wa kwanza kushoto).

UPO HAPO !!!


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mh. William Lukuvi akimshauri Bw. Saidi ambaye ni dereva wa Taxi wa Temeke,afanye mazoezi na apate lishe bora ili aweze kufuza huo mwili wake huku kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar,Afande Suleiman Kova akisisitiza jambo katika hilo.hii ilikuwa ni siku ya ukaguzi wa taxi zote hapa mjini ikiwa ni pamoja na kupigwa mkorogo ubavuni mwa tax.
Kwa hisani ya michuzijr.

Monday, August 24, 2009

KATUNI YA LEO


WATANGAZAJI MACHACHARI BONGO

Watangazaji mahiri hapa nchini Kulia ni Maimartha wa Jesse kutoka East Africa Television (EATV Channel 5) na shoto Saida Mwilima wa Star TV wakiwa na Khadija Mnoga (kati) wakati wa onyesho la utambulisho wa bendi ya Extra Bongo jana katika ukumbi wa msasani Club.
Picha kwa hisani ya Pwani raha.com

Sunday, August 23, 2009

BREAKING NEWS !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE ZINASEMA WANAFUNZI 12 WA SHULE YA SEKONDARI IDODI MKOANI IRINGA WAMEFARIKI DUNIA HAPOHAPO NA WENGINE KADHAA KUJERUHIWA BAADA YA BWENI LAO KUSHIKA MOTO.HABARI YA VIFO NA MAJERUHI IMETHIBITISHWA NA KAMANDA WA POLISI MKOANI HUMO.

MREMBO WA WIKI

Saturday, August 22, 2009

MATUKIOUK TUNAWATAKIA WADAU WOTE ULIMWENGUNI " MFUNGO MWEMA" KATIKA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI

MICHAEL JACKSON HAD A GAY LOVER

Michael Jackson had a secret male lover when he died.
A man claiming to be the late singer's boyfriend says he has been left heartbroken after their "short romantic love story" ended tragically when the 50-year-old singer died from a suspected cardiac arrest in June.
Skin clinic worker Jason Pfeiffer - who is employed by Michael's dermatologist Dr. Arnold Klein - says he feels "empty" without the singer.
He said: "I've lost my soulmate. It's very hard to describe the loss I feel - but there is something that's empty in my heart.
"It was a short romantic love story that ended in tragedy."
Jason, 35, claims they first became friends during a series of telephone conversations, which evolved into secret late night trysts in his car when Jackson asked for a lift home.
I've lost my soulmate. It's very hard to describe the loss I feel - but there is something that's empty in my heart.
It was a short romantic love story that ended in tragedy.
He said: "I guess our first 'date' was in my car. We went for a drive and were talking and having fun, but Michael had his minders who were 'nosey' as Michael put it.
"We had to make sure we were not caught, and although the date was short as I had to take him home before anyone noticed, we had a great time. I thought nobody else knew, but have since discovered that others did surmise the truth."
Overweight Jason claims he was in regular contact with the 'Thriller' up until his death.

He says he became concerned when Michael started acting strangely and claims the 'King of Pop' had started saying goodbye to friends and loved-ones.
He told Australian magazine Woman's Day: "He completely changed in the final two weeks. He was overly religious, overly dramatic, exhausting and exhausted. He was saying goodbyes the week before passing. Everyone was creeped out by it.
"Michael got very retrospective in the last few weeks, he was talking about God and the Mayan calendar and the year 2012 - which is when the Mayan calendar ends."
Meanwhile, the date of Jackson's burial has been postponed.
His father Joe Jackson is now unsure when the ceremony will take place and says it is unlikely to take place at Los Angeles' Forest Lawn Memorial Park on what would have been the star's 51st birthday on August 28 as previously planned.
Joe said: "I don't know now. We have to figure it out."
It has also been announced the movie created from rehearsal footage of Michael's planned 'This Is It' tour will only be shown at cinemas for two-weeks.
Sony has confirmed 'Michael Jackson: This Is It' will be released on October 28 for a fortnight, and tickets will go on sale one month earlier.

Friday, August 21, 2009

PARTY YA CLOUDSFM JANA MOVENPICK

Gerald Hando, Ray C and Gardner
Marlow with a fan.

Kanumba with Aunt Ezekiel


Jesse ,Baraka and Tume



Ado ,Rita and Kinje




Pipi,P-Funk ,Rita and Sara





Hasheem Thabit with friends.


Picha kwa hisani ya http://www.fullshangwe.blogspot.com/



Thursday, August 20, 2009

HASHEEM THABIT AALIKWA NA JK IKULU

Thabit akiingia Ikulu
Rais JK akiwa na Familia ya Hasheem Thabit Ikulu alkowaalika kwa chakula cha mchana majuzi.
Picha na Fred Maro wa Ikulu.

Wednesday, August 19, 2009

TUMPIGIE KURA DIVA WETU TEDDY KALONGA


Mtanzania Teddy Kalonga kwa mara nyingine tena anabeba bendera yetu ughaibuni na hivi sasa amekuwa ni mmoja wa warembo wanaowania nafasi ya kuwa mtangazaji Luninga ya SPIKE TV.SPIKE TV ni channel ya Michezo ya wanaume huko Marekani.Teddy anatakiwa kupigiwa kura ili ashinde nafasi hiyo ambayo mwenyewe anasema hajawahi kuifanya maishani na anafurahi akiipata na kuahidi kulitangaza vyema jina la Tanzania.“well, nilienda kufanya interview sikujua kama kutakuwa na mambo ya picha au competitions, ila ndio hivyo nimekuwa mmoja wa washindani” alisema Teddy alipoongea na Spoti Starehe leo. aidha nilimuuliza Teddy kama Channel hiyo inahusika na mambo gani ni michezo tuu ama naye alisema”…mambo mengi kama the most shocking reality things, cars, I mean vitu vingi vinavyopendwa na wanaume mostly”.

ASKOFU MAYALLA AFARIKI DUNIA

ASKOFU mkuu wa jimbo kuu la Mwanza, kanisa Katoliki Mhashamu Anthony Petro Mayalla (69) amefariki dunia leo mchana kutokana na maradhi ya moyo baada ya kuugua ghafla akiwa ofisini kwake.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mkurungenzi wa mawasiliano wa baraza la Maaskofu (TEC) kanisa katoliki, Padri Revocatus.Makonge Askofu huyo amefariki baada ya madaktari wa Hospitali ya rufaa ya Bugando kuhangaika kumpatia matibabu bila ya mafanikio.

Alisema kuwa marehemu aliamuka salama leo na kuendelea na shughuli zake za kila siku ofisini kwake mpaka majira ya saa 4:00 asubuhi ambapo alizidiwa ghafla na kukimbizwa Hospitali ya rufaa ya Bugando.Habari kutoka katika ofisi ya aksofu huyo, zimeeleza kuwa alipatwa na maradhi hayo wakati akiwa katika maandalizi ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Vatican ambaye alikuwa akitarajiwa kufanya ziara jimboni kwake Oktoba 5 mwaka huu kwa ajili ya kufungua ujenzi wa hospitali ya watoto.“Baada ya kufikisha hospitalini hapo madaktari waliahangaika kuokoa maisha yake lakini nahati mbaya lifariki dunia majira ya saa 8;30 mchana,” alieleza Padri Revocatus Makonge.

Askofu Mayalla alizaliwa Aprili 23 mwaka 1940 katika katika kijiji cha Nera wilayani Kwimba na kupata elimu yake ya msingi katika wilaya hiyo na masomo ya sekondari.Askofu Mayalla alikuwa amehitimu shahada ya kwanza ya elimu aliyopita katika chuo kikuu cha Loyola huko Chicago Marekani mwaka 1973 hadi 1975. Frederick Katulanda, Mwanza.

RISASI MCHANGANYIKO


ANGALIA MIJI YETU ILIVYO MIZURI

DAR-ES-SALAAM(BONGO) MWANZA (ROCK CITY)





MR & MRS CARTER

Dinner date: Beyonce looked red hot next to her casually-dressed husband as they dined at Gils restaurant and lounge in Dubrovnik's Old city.

Tuesday, August 18, 2009

SPIKA SITTA MOTONI DODOMA

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta, jana jioni alilazimika kuwaomba radhi wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kunusurika na hatari ya wazi ya kupoteza uanachama iliyoanza kujionyesha tangu juzi jioni.
Hatua hiyo ya Sitta kuomba radhi ilikuja baada ya wajumbe takriban wote wa vikao viwili vya juu vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) vya chama hicho kujenga hoja za kumshambulia wakipinga namna anavyoliendesha Bunge katika mwelekeo wa kukidhalilisha chama hicho na serikali yake.
Habari za uhakika kutoka ndani ya vikao hivyo vilivyokuwa vikifanyika katika Ukumbi wa Mlimani mjini hapa tangu juzi, zinaeleza kwamba, takriban wajumbe wote waliokuwa wakisimama kuzungumza katika vikao hivyo walikuwa wakitaka kuona Sitta akipokonywa uanachama wa chama hicho, ili liwe fundisho kwake binafsi na wana CCM wengine.
Taarifa kwamba Sitta angeomba radhi zilianza kusikika tangu jana asubuhi baada ya wajumbe kadhaa wa vikao hivyo kuieleza Tanzania Daima kwamba spika huyo alifanya kikao na Rais Kikwete kabla ya NEC kuanza.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha siri kati ya rais na Sitta zinaeleza kwamba, mwenyekiti huyo wa CCM alimtaka kiongozi huyo kutafakari kwa makini tuhuma zote zilizokuwa zikielekezwa kwake na kutoa utetezi ambao utamuepusha katika hatari ya kupokonywa kadi ya uanachama na hatimaye uspika wake.
“Kuna taarifa kwamba Rais Kikwete alipokutana na Sitta leo asubuhi (Jumatatu), alimuomba kiongozi huyo atumie busara kulimaliza suala hilo ambalo hatima yake ingeweza kuwa mbaya,” alisema mjumbe mmoja.
Tukio hilo baya kabisa kuwahi kumfika Sitta ambaye amekuwa akijinadi kuwa ni spika wa kasi na viwango, lilihitimishwa na uamuzi wa NEC kuunda kamati maalumu kuchunguza kiini cha kufikia hapo.
Habari kutoka ndani ya vikao hivyo vya CCM, zinaeleza kuwa, kamati hiyo maalumu itaongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na wajumbe wake wengine watakuwa ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Pius Msekwa na mwanasiasa mkongwe, Abdulrahman Kinana.
Kwa mujibu wa habari hizo, mwelekeo wa wana CCM hao kutaka kumwadhibu Sitta ambaye katika siku za hivi karibuni amejizolea umaarufu wa kisiasa ndani na nje ya Bunge, hata kuwa na uwezo wa kumnyoshea kidole mtu au taasisi yoyote, ulianza kujitokeza tangu katika Kamati Kuu juzi.
Hali hiyo ya mambo, ilimlazimu Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuwaomba wajumbe wa CC, wamruhusu kuipeleka ajenda hiyo ya Sitta katika kikao cha NEC kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa uamuzi.
Mjadala huo ulipoanza ndani ya NEC, wajumbe takriban wote waliokuwa wakizungumza walionekana kumshutumu Sitta wakihoji namna anavyoliendesha Bunge katika misingi isiyozingatia taratibu na kanuni za mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola.
“Jana na leo ni siku mbaya na ngumu kwa Sitta, kwani kati ya wajumbe zaidi ya 40 waliozungumza, ametetewa na wajumbe watatu tu, ambao wote waliposimama kuzungumza walikuwa wakizomewa hata kusababisha mwenyekiti kuingilia kati na kutaka hali ya utulivu,” alisema mmoja wa wajumbe ambaye alionekana dhahiri akiwa upande uliokuwa ukimshambulia spika huyo.
Habari zaidi zinasema, mjumbe mmoja alisimama na kumshutumu Sitta kuwa ndiye chimbuko la kuongezeka kwa ufa wa makundi ndani ya chama hicho, kutokana na tabia yake ya kuliendesha Bunge akiwa ameambatana na kundi moja la wabunge wanaomuunga mkono.
Mjumbe huyo (jina tunalo), alifikia hatua ya kusema Sitta ameanzisha kikosi cha wabunge wake (aliowaita first 11) ambao siku zote amekuwa akiwapanga kuzungumza wakiwalenga watu fulani na wakati mwingine kuirarua serikali bungeni kwa sababu tu ya kutimiza malengo yao binafsi.
Mbali ya huyo, mjumbe mwingine kati ya wajumbe zaidi ya 50 waliozungumza tangu juzi, alifikia hatua ya kufananisha mashambulizi hayo na kitendo cha wawindaji kumjeruhi nyati na kumwacha pasipo kumuua kabisa, akisema ni cha hatari kwa maisha ya wawindaji.
Wajumbe wa NEC waliozungumza na Tanzania Daima wanasema, mjumbe huyo alifikia kutoa matamshi hayo, lengo likiwa ni kukitaka kikao hicho cha NEC kuhitimisha mjadala mzima wa juzi na jana kwa kumpokonya kadi ya uanachama kiongozi huyo.
Habari zaidi zinaeleza kuwa, mjumbe mwingine aliyekuwa akiunga mkono hoja hiyo alifikia hatua ya kusema, CCM haiwezi kutikisika iwapo Sitta atapokonywa uanachama, akisema katika wakati tofauti chama hicho kimepata kupoteza makada maarufu katika siku zilizopita.
Kwa mujibu wa mjumbe huyo, makada wengine wa chama hicho aliokuwa akiwazungumzia walikuwa ni aliyekuwa Makamu wa Rais, Aboud Jumbe, ambaye mwaka 1984 alivuliwa wadhifa wake na NEC, baada ya kuvuja kwa taarifa zilizokuwa zikimhusisha na mipango ya kuudhofisha muungano.
Mwingine aliyetajwa katika kundi hilo ni Maalim Seif Sharif Hamad na wana CCM wengine 16 wa Zanzibar ambao walivuliwa uanachama mwaka 1988, wakituhumiwa kukihujumu chama hicho na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Kada wa tatu wa chama hicho aliyelazimika kukihama chama hicho akiwa na umaarufu aliyetajwa na mjumbe huyo kuwa mfano wa watu walioondoka CCM na kukiacha kikiendelea kuwa imara, ni Augustine Mrema, ambaye aliondoka mwaka 1995 kutokana na kuhitilafiana na serikali na aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, Cleopa Msuya, akamshauri rais amfukuze kazi.
Wakati mjumbe huyo akitoa matamshi hayo, mjumbe mwingine aliitaka NEC kutohofia uamuzi wa kumvua Sitta uanachama, akitaka wajumbe wajifunze kutoka nchini Afrika Kusini ambako chama tawala kilifikia hatua ya kumvua madaraka rais wa nchi (Thabo Mbeki) na bado kikajihakikishia ushindi uchaguzi mkuu ulipoitishwa tena.
Mjumbe mwingine wa CC na NEC aliyezungumza na Tanzania Daima jana alisema, mwelekeo wa vikao hivyo, zilikuwa ni salamu tosha kwa Sitta na makamanda wenzake wa ufisadi wakati huu chama hicho kinavyojiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwakani.
“Huyu jamaa (Sitta) na wapambe wake wamekuwa wakikivuruga chama na serikali ndani na nje ya Bunge kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, kwa kisingizio cha ufisadi. Leo hii wamejionea wenyewe namna damu ya watu waliowaonea kama Edward Lowassa na wenzake inavyowalilia,” alisema mjumbe huyo aliye karibu kimtazamo na waziri mkuu huyo aliyejiuzulu Februari mwaka jana baada ya jina lake kuhusishwa katika sakata la Richmond.
Wakati mjumbe huyo akitoa maoni hayo, mwingine aliyezungumza na gazeti hili alisema, mtiririko mzima wa hoja ndani ya vikao hivyo, unaonyesha namna kundi moja la watu wenye fedha lilivyojipanga kuhakikisha linammaliza Sitta kwa kutumia kila mbinu.
Hata hivyo, habari zaidi kutoka ndani ya vikao hivyo zinaeleza kwamba, kikubwa kilichoonekana kumfikisha Sitta hapo alipo ni namna ambavyo amekuwa akilishughulikia sakata la Richmond na mengine yanayohusu ufisadi ndani na nje ya Bunge.
Baadhi ya wajumbe waliozungumza na Tanzania Daima ambao walieleza kutoridhishwa na namna suala la Sitta lilivyoshughulikiwa, walisema kwa jinsi mjadala ulivyokuwa ukienda, wachangiaji wote ni kama vile walipangwa kummaliza Sitta, kwa madai kuwa amekuwa akiruhusu mijadala inayokimaliza chama kwa hoja ya kupambana na ufisadi.
Wajumbe hao walielezea wasiwasi wao kuwa endapo Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais Kikwete angekubaliana na matakwa ya wajumbe wengi ya kutaka Sitta apokwe uanachama, hali hiyo inaweza kuibua tatizo kubwa, si nchini tu, bali pia kimataifa.
Nje ya Ukumbi wa White House ambako mkutano huo ulikuwa ukiendelea, vikundi vya baadhi ya wajumbe walionekana kutofautiana kuhusu suala hilo, kwa madai kuwa limeibuliwa kwa makusudi na watu wachache wenye ushawishi kifedha ili kupunguza makali ya Sitta.

TEYANNA & RIHANNA ..............

The America’s Most Wanted Tour featuring Weezy, Soulja Boy, Jeezy & Pleasure P stopped in Southern California this past weekend and a few interesting things popped off. While at dinner, I got tipped off that both Teyana Taylor & Rihanna were backstage at the show and my first response was “WHAT? Together?” interesting… After numerous outlets claimed that Teyana was a “Rihanna knock off” as well as attempting to link her with Chris Brown, I was surprised to see the two were buddy buddy! Later that night Teyana linked up with Chris Brown, Polow Da Don and a few other folks at the skating rink but no word on whether Rihanna tagged along.
Which leads me to another small piece of gossip; Some caller by the name of Jaden called in to Power 92.1 in Richmond recently and claims he saw Chris Brown picking Rihanna up from Richmond International Airport last Sunday at 7pm. He says that Chris rode up in a blue lamborghini followed by a silver Range Rover and scooped Rihanna up from the airport before speeding off. [Listen Here]. The only problem with this story is that photos of Rihanna kissing a DJ at the Pink Elephant were released that same night. So either this guy is lying or those photos were released to contradict anyone who may have spotted them in VA going against the court’s order. hmmmmm….

SOURCE: nicole Bitchie

ACP ZOMBE !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Watu hawawezi kuamini wengine wamenuna wengine wanalia. Lakini Ukweli ni kwamba kuna wachache wanaochekelea kusikia kamanda Zombe kaachiwa huru kwa mashitaka ya mauaji na si yeye tu bali washtakiwa wote.Alipotoka nje ya mahakama alilakiwa kama shujaa na baadhi ya watu wakiwamo maaskari ingawa wengie walikuwa wamenuna kichizi.Ukweli ni kwamba yuko huru na ameondoka kama kamanda wa polisi (RPC) ulinzi kibao huku akiwa na ulinzi wa kimulimuli cha polisi na msafara wa watu kibao. Kweli sheria Msumeno

HABARI ZAIDI NA PICHA : http://www.mpoki.blogspot.com/

Monday, August 17, 2009

ZOMBE ARUDI URAIANI AKIWA HURU

BREAKING NEWS:

ALIYEKUWA MKUU WA UPELELEZI WA JESHI LA POLISI MKOA WA DAR-ES -SALAAM (ACP) ABDALLAH ZOMBE NA WENZAKE WANANE WAMEACHIWA HURU NA MAHAKAMA KUU .
HABARI ZAIDI ZINAFUATA

KATUNI YA LEO


MAWAZIRI WAKUU WA TANZANIA TOKA UHURU

MIAKA 10 tangu kifo chake,Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ameongoza kwa ubora miongoni mwa mawaziri wakuu 10 waliowahi kushika wadhifa huo nchini, akifuatiwa kwa karibu na Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo Pinda.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa miezi mitatu iliyopita na Kampuni ya Synovate ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kama Steadman Group Tanzania, Pinda ametofautiana kwa pointi moja tu nyuma ya mwalimu Nyerere.
Mwalimu Nyerere anaongoza kwa asilimia 29 na Pinda anamfuatia kwa asilimia 28 na kuwaacha wengine kwa tofauti kubwa akiwamo aliyemtagulia Edward Lowassa. Mawaziri wakuu wanaoshika mkia kwa ubora ni John Malecele, Cleopa Msuya na Joseph Warioba ambao kila mmoja amepata asilimia moja.
Hayati Edward Sokoine, ambaye alikufa kwa ajali ya gari mwaka 1984 akiwa ana sifa kemukemu kutokana na kuongoza vita dhidi ya walanguzi na wahujumu uchumi, anashika nafasi ya tatu kwa ubora akiwa na asilimia 26.
Baada ya Sokoine ambaye anashika nafasi ya tatu, mawaziri wakuu wengine wamepata alama za ubora chini ya asilimia 10.
Nafasi ya nne inashikiliwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kwa asilimia sita wakati Edward Lowassa ambaye alijiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond mwaka jana, anafungana na Mzee Rashid Kawawa na kushika nafasi ya tano kwa kuwa na asilimia nne.
Nafasi ya tano inashikiliwa na Dk Salim Ahmed Salim ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ambao kwa sasa unajulikana kama Umoja wa Afrika (AU).
Utafiti huo unamuonyesha pia Pinda kama waziri mkuu anayefahamika zaidi kwa watu kuliko wengine. Katika kundi hilo, Pinda anafahamika kwa watu kwa asilimia 81, akifuatiwa na Lowassa kwa asilimia 73.
Wanaofuatia pamoja na kiwango cha asilimia cha kufahamika ni Sumaye (60), Sokoine (45), Nyerere (37), Kawawa (34) Malecela (24), Warioba (20), Msuya (18) na Dk Salim (14).
Meneja Msaidizi wa Synovate, Agreey Orio aliviambia vyombo vya habari hivi karibuni kuwa kwenye utafiti huo Rais Jakaya Kikwete ana ana nafasi kubwa ya kuchaguliwa tena kwenye nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao, 2010.
Kwa upande wa rais wa Zanzibar, utafiti huo ulionyesha kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, anapewa nafasi kubwa ya kushinda.

SPOTTED


Nicole Scherzinger and Lewis Hamilton were spotted out for a date night at Katsuya in Hollywood on Saturday (August 15).
With the Pussycat Dolls beauty decked out in a flowing sheer dress while her racer beau dressed in all-black, the pair smiled and held hands while walking past paparazzi following their meal.

Friday, August 14, 2009

KIMWANA WA WIKI


MAOFISA DECI WAACHIWA HURU

HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imewaachia huru kwa dhamana wachungaji wengine wawili wa DECI baada ya kukamilisha masharti.
Wachungaji hao, walioachiwa huru jana na Hakimu Mkazi, Nyigulile Mwaseba mara baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ni Samuel Sifael na Arbogast Kipilimba.
Kabla ya washtakiwa hao kuachiwa huru Wakili Mwandamizi wa Serikali, Justus Mlokozi alidai kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kuomba ipangiwe tarehe nyingine.
Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mwaseba aliiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 9, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
Uamuzi huo unatolewa baada ya Agosti 12, mwaka huu hakimu mkazi, Waliarwande Lema kuwaachia huru viongozi watatu wa Deci mara baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali, Justus Mlokozi kudai kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na hati ya kuomba kuongezewa muda kutoka kwa mkuu wa upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na hati ya kuondoa pingamizi la dhamana kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka chini ya kifungu cha 148 (4) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Waliochiwa kwa dhamana juzi ni Jackson Sifael, Dominick Kigendi, Timoth Sangura ambao wote walikamilisha masharti ya dhamana.
Viongozi hao ambao pia ni wachungaji wa madhehebu ya Kanisa la Pentekoste wanaokabiliwa na mashtaka ya kuendesha na kusimamia mradi wa upatu kinyume cha sheria (DECI).
Akiwaachia kwa dhamana hiyo juzi, Hakimu Lema alisema kutokana na hati iliyowasilishwa mahakamani hapo kutoka kwa DPP chini ya kifungu cha 148(4)cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai inaonyesha kuwa hana pingamizi tena la dhamana dhidi ya washtakiwa hao.
Hivyo aliwataka washtakiwa hao kuwa na wadhamini wawili wanaominika kwa kila mmoja wao na kwamba, mmoja kati ya wadhamini hao awe mkazi wa jijini Dar es Salaam na kila mdhamini asaini bondi ya Sh 10 milioni.
Pia aliwataka wawasilishe hati zao za kusafiria mahakamani, wasitoke nje ya Jiji la Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama na hawaruhusiwi kufanya mkutano wowote ule unaohusiana na mambo ya DECI.

Sunday, August 09, 2009

MSIBA UPANGA , DARESSALAAM


NDUGU JESSE GEORGE MALONGO WA LONDON UINGEREZA ANASIKITIKA KUTANGA ZA KIFO CHA BABA YAKE MPENDWA MZEE MADAHA GEORGE MALONGO KILICHOTOKEA IJUMAA TAREHE 7 SAA MOJA JIONI. MSIBA UKO NYUMBANI KWA MAREHEMU NO.3 NKOMO NA ALYKHAN ROAD UPANGA,DSM MAZISHI YAMEPANGWA KUFANYIKA SIKU YA JUMANNE JIONI MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DSM .

TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AIPUMUZISHE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI

Saturday, August 08, 2009

SYLIVIA SHALLY AWA MISS ILALA 2009


Miss Ilala 2009-2010 Sylivia Shally (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Gladis Shaoluja (kushoto) pamoja na Evelyn Gamasi ambaye alifanikiwa kushika nafasi ya tatu warembo wote hao wamefanikiwa kuingia katika shindano la kumsaka Miss Vodacom Tanzania 2009-2010.

Thursday, August 06, 2009

ALIKIBA KUTUMBUIZA CLUBAFRIQUE SEP 25


REAL MEN !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


MAENEO NYETI BONGO KUWA GIZANI KWA SIKU TANO

MAKAZI ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete, yatakumbwa na giza kwa muda wa siku tano mfululizo, kutokana na kuharibika kwa transfoma kubwa ya vituo vya Masaki na Oysterbay, inayosambaza umeme katika maeneo hayo nyeti.

Maeneo hayo yatakuwa gizani kuanzia Agosti 22 hadi Agosti 26, ambapo kutakuwa na matengenezo makubwa katika transfoma ya kituo cha Masaki.
Taarifa iliyotolewa jana na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, Badra Masoud, ilisema kuwa maeneo hayo yatakosa umeme, kwani matengenezo yake yatalazimisha kufumuliwa kwa transfoma nzima na haiwezi kuwashwa tena baada ya kazi hadi itakapotengemaa.
“Ubovu wa vituo hivyo vya transfoma, utasababisha maeneo hayo kukosa umeme kwa muda wa siku tano kutokana na matengenezo makubwa yatakayoanza Agosti 13 hadi 17, mwaka huu katika kituo cha Oysterbay na Agosti 22 hadi 26 katika kituo cha Masaki.
“Matengenezo yatafanyika usiku na mchana ili kukamilisha shughuli hiyo kwa muda uliopangwa, hivyo kuepusha usumbufu wa ziada kwa wateja,” alisema Badra katika taarifa hiyo.
Alisema shirika linalazimika kuifanya kazi hiyo sasa, kwa sababu ya usumbufu mkubwa ambao wateja wa maeneo haya wamekuwa wakiupata kutokana na ubovu huo.
Hata hivyo aliwahakikishia wateja wa maeneo hayo kuwa baada ya matengenezo watapata huduma bora ya umeme.

Mbali na Ikulu na makazi ya Waziri Mkuu, taarifa hiyo iliyataja maeneo mengine yatakayokumbwa na kadhia hiyo kuwa ni ofisi za Ubalozi wa Afrika Kusini na Nigeria, Shule ya Kimataifa ya Tanganyika na baadhi ya nyumba za mawaziri zilizoko eneo la Masaki.
Maeneo mengine ni baadhi ya hoteli za kitalii kama Slipway, Sea Cliff, Golden Tulip, Coco Beach, Coral Beach Club, Yatch Club, Hoteli Karibu, Oysterbay Hotel, Msasani Peninsular na TPDF Masaki.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, maeneo mengine ni pamoja na Barabara ya Kenyatta, Barabara ya Tumbawe, Barabara ya Hill, Mtaa wa Kajificheni, josho la mbwa, nyumba za bandari, Kahama Mining, Toure Drive, Barabara ya Haile Selasie, Barabara ya Chole na eneo la Kanisa la St Peter, vijiji vya Onella, Valhalla, Morogoro Store na Baobao.

Kuhusu maeneo yatakayoathirika kutokana na kuharibika kwa transfoma ya kituo cha Oysterbay yatakayokosa umeme kuanzia Agosti 13 hadi Agosti 17 mwaka huu, taarifa hiyo iliyataja kuwa ni Kinondoni Hananasifu, Moscow, Mkwajuni, Mwananyamala, Ada Estate, nyumba za TANESCO, Drive Inn, Victoria na maeneo ya jirani, Uporoto, Namanga, Msasani Magunia, Barabara ya Kimweri, Karume, Mwananyamala kwa Kopa na Kwale, pamoja na maeneo yanayozunguka mnara mkuu wa Vodacom na Barabara ya Ali bin Said.
Mengine ni Polisi Oysterbay, Barabara ya Laibon, Chunyu, Kenyatta, balozi za Japan, Urusi, India, Kenya na Ufaransa, Barabara ya Kinondoni, ikiwamo Stanbic Bank, Barabara ya Kaunda, Hospitali ya CCBRT na maeneo ya jirani.

Wednesday, August 05, 2009

WANENE WA WIZARA YA AFYA

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. Davidi Mwakyusa akizungumza na Naibu Waziri wa Afya Dkt Aisha Kigoda(katikati) na katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Blandina Nyoni (kulia) mara baada ya uzinduzi wa mabaraza ya Wataalam wa Huduma za Maabara za Afya na Wataalam wa Radiolojia leo jijini Dar es salaam.

Picha na Aron Msigwa- MAELEZO

WAZAIRE MPO HAPO ? BONGO KAMA KINSHASA







KATUNI YA LEO


Tuesday, August 04, 2009

SARA'S KITCHEN PARTY

THE AFRICAN QUEEN LOOKING FABOULOUS
CLOSE FRIENDS

BENKI KUU YAONYWA


Na Ramadhan Semtawa

SERIKALI imeonya Benki Kuu (BoT), isithubutu kutoa kiasi cha fedha takriban Sh 60 bilioni kwa mfanyabiashara Devram Valambhia, nje ya mahakama.
Onyo la serikali kwa BoT limekuja wakati kumekuwa na shinikizo la Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, kutaka BoT imalize kesi hiyo ya Valambhia nje ya mahakama kwani tayari imetumia kiasi cha Sh 8 bilioni za uwakili hadi mwaka jana Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), alivyofanya ukaguzi.
Wakati kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, ikitoa msimamo huo kurejea ule wa Kamati ya Fedha na Uchumi, Gavana wa BoT Profesa Benno Ndulu, ametoa msimamo akisema tayari wamepata maelekezo ya serikali yakionya benki hiyo isitoe fedha zake kwa Valambhia nje ya mahakama.
"CAG alionesha wasiwasi kuwa pesa ambazo wakili alilipwa zilikuwa ni nyingi mno kulingana na kesi yenyewe. Kesi yenyewe inagharimu Dola za Marekani 55 milioni na mpaka ukaguzi unafanyika wakili alikuwa amelipwa Sh 8 bilioni," ilisema kamati ikisisitiza umuhimu wa kesi hiyo kumalizwa nje ya mahakama.
Valambhia anaidai serikali kiasi cha dola 55 milioni kutokana na kuiuzia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, magari kutoka Chekoslovakia.
Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu ofisini kwake jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, gavana Ndulu alisema tayari wamepata maelekezo hayo ya serikali ikionya fedha zake zisiguswe.
"Serikali yenyewe ambayo ndiyo yenye fedha zake, imekataa tusilipe nje ya mahakama..., kwa hiyo ndiyo msimamo uliopo sasa tunaoutekeleza," alifafanua gavana. Gavana alisema BoT siyo yenye dhamana ya kulipa fedha za Valambhia, kwani yenyewe inahifadhi fedha za watu ambazo ni za serikali.
Akifafanua, gavana alisema kama serikali ikitoa idhini BoT haitakuwa na pingamizi, lakini hadi sasa haiwezi na wala haina mpango wa kulipa fedha hizo nje ya mahakama.
"Mwenye pesa kakuonya usiguse fedha zake halafu mwingine aje akwambie uzichukue ukamlipe mtu, hapana... hatwendi hivyo," alisisitiza. Kwa msisitizo, alisema anafahamu lipo shinikizo kutoka kwa watu mbalimbali ambao (ukiacha Kamati ya Bunge), wana maslahi yao.
"Najua kuna watu wanashinikiza hili kwa maslahi yao binafsi, tunawajua, lakini msimamo ni kwamba, I can't do that (siwezi kufanya hivyo)," alisisitiza gavana.
Kamati hiyo ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika taarifa yake ya kwanza mwaka huu, imeitaka BoT kumaliza kesi hiyo nje ya mahakama ili kuepuka gharama zaidi za uendeshaji kesi kwa kulipa mawakili.
Hata hivyo, BoT iliijulisha kamati kuwa ilisitisha mkataba na Kampuni ya Mkono tarehe 22 Januari mwaka 2008 na kuteua kampuni nyingine ya Uwakili ya Law Associates, kuitetea BoT katika kesi zake zote.
Sehemu ya taarifa ya kamati ilisema, "Kamati ilifuatilia agizo la Kamati ya Fedha na Uchumi ililolitoa kwa Benki Kuu mwaka 2007 kuhusiana na malipo makubwa ya ada kwa kampuni ya uwakili ya Mkono and Company Advocates. Malipo haya yalitokana na kesi iliyokuwa na inayoendelea mahakamani kati ya Benki Kuu na ndugu Devram Valambhia."
"Kesi hii ni ya siku nyingi sana na inatokana na uamuzi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kununua magari kutoka nchini Chekoslovakia."
"Kamati iliona kuwa ni vema kesi hii ikamalizwa nje ya mahakama kwani iwapo itachukua muda mrefu zaidi gharama za kesi zitazidi thamani ya kesi yenyewe. Kamati ya Fedha na Uchumi iliiagiza Benki Kuu kufanya mazungumzo na kampuni ya Mkono ili kupunguza gharama za kesi na hatimaye kuimaliza kesi hiyo nje ya mahakama.
Hata hivyo, kamati ilifafanua kwamba inakubaliana na uamuzi wa BoT kusitisha mkataba na kampuni ya uwakili ya Mkono, lakini ikasisitiza iwapo juhudi hazitawekwa kumaliza kesi hiyo ya Valambhia nje ya mahakama, kampuni ya uwakilii iliyopewa kazi hiyo nayo italipwa fedha nyingi na kwenda zake na ikawa ni mtindo wa mawakili kufaidika na kesi za BoT ambazo haziishi.

MIRIAM MAKEBA'S TRIBUTE CONCERT ON 10/08/2009


Miriam Makeba’s Tribute Concert will be held on August 10 from 11am on the Mary Fitzgerald Square in Johannesburg.
Artists such as Oliver Mtukudzi, Dorothy Masuka, Abigail Kubheka, Sibongile Khumalo, Yvonne Chaka Chaka, Siphokazi, Deborah Fraser, Makeba’s Band, HHP and Guinea’s super drummer, Pap Kouyate, will entertain the crowds.
Makeba,who’s been hailed as one of the greatest african musicians, died on stage in November 2008 while performing in Italy.

Monday, August 03, 2009

POZI !!!

Vivica J. Fox

SPOTTED

Basketball player Carmelo Anthony and fiance Lala Vazquez were spotted shopping at Malibu Lumber Yard and James Perse this weekend in California. According to the paps, the duo didn’t look too happy with each other.
SOURCE : CL