MWANAUME mmoja nchini Kenya amenusurika kuuawa na chatu baada ya kumng'ata nyoka huyo kabla ya kuomba msaada kwa kutumia simu yake ya mkononi katika mapambano yaliyodumu kwa muda wa saa moja.
Ben Nyaumbe, ambaye ni mkulima, alifikwa na mkasa huo mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya chatu huyo aliyekuwa mawindoni, kumnasa shambani kwake eneo la Malindi mwambao mwa Bahari ya Hindi.
"Nilikanyaga kitu kinachofanana na sponji na ghafla mguu wangu ukawa umezungukwa na chatu mkubwa," alisema Nyaumbe na kuongeza:
"Wakati chatu huyo akiwa amejiviringisha mwilini mwangu, niliamua kujiokoa kwa kumng'ata meno."
Alisema baada ya kumng'ata, chatu huyo alimburuza hadi kwenye mti na baadaye kujilegeza, jambo ambalo lilimwezesha kuchukua simu yake ya mkononi iliyokuwa mfukoni na kuomba msaada.
"Baadaye akaja msimamizi wa shamba na polisi na kumfunga chatu huyo kwa kamba kisha kumvuta huku mimi nikiwa nakifunga kichwa chake kwa shati langu," alieleza.
"Baadaye wote tukaanguka chini na tukawa tunahema," alieleza Nyaumbe ambaye hata hivyo alipata majeraha mengi kwenye ulimi na kuchubuka sehemu mbalimbali za mwili. Alisema chatu huyo alifumuka kwenye mti aliojiviringisha na kukimbia.

No comments:
Post a Comment