.

.

.

.

Wednesday, April 15, 2009

KIKWETE ACHAMBUA WAKUU WA MIKOA

RAIS Jakaya Kikwete amebadilisha vituo vya kazi kwa Wakuu wa mikoa 11 ambapo
Wiliam Lukuvi anakuwa mkuu wa mkoa wa DSM
Abbas Kandoro anakwenda kuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Taarifa iliyotolewa jana Dar es Salaam na Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa imesainiwa na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri, lengo la mabadiliko hayo ni kutoa msukumo zaidi wa shughuli za serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. James Msekela anahamia Dodoma.
Enos Mfuru kutoka Kagera kwenda Mara,
Issa Machibya kutoka Mara kwenda Morogoro,
Said Kalembo kutoka Morogoro kwenda Tanga,
Mohamed Abdulaziz kutoka Tanga kwenda Iringa
Amina Mrisho kutoka Iringa kwenda Pwani.
Wengine ni Dk. Christine Ishengoma kutoka Pwani kwenda Ruvuma,
Monica Mbega kutoka Ruvuma kwenda Kilimanjaro
Mohamed Babu kutoka Kilimanjaro kwenda Kagera.
Mabadiliko hayo ya wakuu wa mikoa yamefanyika wiki tatu tangu Rais Kikwete afanye uteuzi wa wakuu wa wilaya kwa kuteua wapya 15

No comments:

Post a Comment