.

.

.

.

Sunday, October 23, 2011

NI JESTINA GEORGE .......................


Jestina akiwa amevalia vazi liliobuniwa na KIKI wa Kiki's Fashion Tanzania
Jestina akienda kupokea tuzo baada ya kutangazwa Blog of the year
Jestina akimwaga speech kuwashukuru wote waliompigia kura na kumsupport
Zulfa, Jestina, Lynn & Frank kutoka Urban Pulse wakifurahia ushindi
Jestina akiwa na mdogo wake Luiza baada ya kupokea tuzo
Jestina akiwa na marafiki zake waliokwenda kumsupport kutoka kushoto Jacque Maina, Jestina, See Li, Amina & Zulfa musa
Frank Eyembe kutoka Urban Pulse, Lynn Kapinga, Jestina George, Mashel & Musa Sissasi Sarr

Jestina akiwa katika pose na Tuzo yake
*******************
Salam,

Urban Pulse Creative inapenda Kumpongeza dada yetu Jestina George kwa kushinda tuzo muhimu ya Blog ya Mwaka katika tuzo za BEFFTA zilizizofanyika Jumamosi tarehe 22 Octoba 2011 ndani ya ukumbi wa Lighthouse, Camberwell jijini London.

Wakati akitoa Hotuba yake Jestina alianza kwa kumshuru Mungu ambae amemwezesha kumpatia uzima, afya njema pamoja na mafanikio makubwa aliyopata mwaka huu. Aliendelea kwa kuwashukuru Wazazi wake na mwisho wadau wote ambao walimpigia kura Pia Mabloggers na Tovuti mbalimbali ambazo zimemsaidia kumpigia debe na kuibuka mshindi wa BLOG OF THE YEAR 2011 kutoka kwenye kundi lenye Blog 15 za kimataifa. Hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Mtanzania kuingia, kushinda na kumfanya kuwa Mtanzania wa Kwanza kupokea tuzo za BEFFTA kwa upande wa Blogs

Jestina George ameitoa wakfu Tuzo yake kwa dada yake mpendwa Kissa George ambaye hatunaye tena hapa Duniani.

Vazi lake lilibuniwa na KIKI wa Kiki's Fashion Tanzania. Kwa maelezo zaidi na taswira mbalimbali za tukio hili Tembeleahttp://missjestinageorge.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment