.

.

.

.

Sunday, May 20, 2012

MIRIAM ODEMBA NA KANYE WEST WAMNYIMA RAHA KIM KARDASHIAN

NANI alijua kuwa hata wanawake wazuri kama Kim Kardashian nao huwa wanateswa na wivu, basi amini usiamini Miriam Odemba alimnyima raha mlimbwende huyo baada ya kuwa bega kwa bega na 'boy frend' wake, Kanye West.

Inadaiwa kuwa Kim alianzisha patashika nyuma ya jukwaa wakati mpenzi wake huyo akizindua nguo zake mpya huko Ufaransa.

Kim na Kanye walikuwa Paris kwa shughuli hiyo na Odemba yuko huko Ufaransa kwa kazi yake ya kuonyesha mavazi.

Inasemekana Odemba aliwahi kukutana na Kanye West na kujuana mwaka jana wakati rapa huyo akizindua nguo za kwanza huko Ufaransa.

Sasa wikiendi hii Kanye West alipokwenda tena Odemba baada ya kumuona rafiki yake, alimchangamkia na kujumuika naye kucheza muziki kitendo ambacho hakikumfurahisha Kim.

Wakati Kanye akicheza na Odemba, Kim alikuwa amekaa na Swizz Beatz na mkewe Alicia Keys, unaambiwa Kim alikuwa hapepesi macho kwa wivu.

Hata hivyo Kim anadaiwa kuwa alishindwa kuendelea kuvumilia kuona mwanamke mrembo akiendelea kucheza na mpenzi wake na kuhatarisha penzi lao changa. Moja kwa moja alimvuta Kanye huku maneno yakimtoka.

Mastaa wengine waliohudhuria shughuli hiyo ni pamoja na 
 D’Banj, P.Diddy, common, Big Sean, Cassie na Waka Flocka Flame.

2 comments:

 1. Tenaaa, mwambie huku kuna warembo bwana.
  Huku hatutegemei pewa wala makeups.
  apite manzese aone wadada ndani ya MT na ZAZUU za kitaa wanavyovutia. Wakimwagwa huko, aaaaaah wameumia. kwhiiiiiiiiiiiii

  ReplyDelete
 2. World famous celebrities information, news, song, award list, movie and lifestyle are there Enjoy famous celebrities most popular song and Movie and know their lifestyle, Biodata,news, contact number and home address Enjoy famous celebrities top and hot photo and video.
  Kim Kardashian

  ReplyDelete