.

.

.

.

Friday, May 02, 2014

CLOUDS MEDIA YAPAA KIMATAIFA

Kampuni ya Clouds Media International leo imetangaza kuwa imepewa leseni ya kurusha matangazo katika nchi za umoja wa falme za kiarabu (UAE). Akielezea kuhusu leseni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bwana Joseph Kusaga, amesema sasa kituo cha Clouds TV kimataifa kitakuwa kikishuhudiwa na watu wa mataifa mbalimbali.
Clouds TV kimataifa ni mwendelezo wa televisheni maarufu sana kwa vijana nchini Tanzania, hata hivyo sehemu kubwa ya maudhui yatakayokuwemo kwenye Clouds TV kimataifa itakuwa na mpangilio mpana wa vipindi kwa watazamaji vitakavyorushwa kwa lugha za Kiingereza na Kifaransa.
Akieleza zaidi Kusaga amesema, “Leo ni siku ya kihistoria na alama ya hatua moja katika mpango wetu wa kina wa kupeleka maudhui ya Clouds TV kimataifa kupitia matangazo kwa njia ya mitandao.”
Clouds TV kimataifa haitotoa tu burudani, lakini pia itakuwa kiunganishi kwa waafrika waishio katika umoja wa nchi za falme za kiarabu pamoja na kuwapa fursa za kutangaza bidhaa zao na kuimarisha uhusiano baina yao. Vituo vya televisheni katika Umoja wa falme za kiarabu vipo vingi na vyenye ushindani mkubwa, lakini Clouds TV kimataifa imebahatika kupata nafasi ya kurusha matangazo yatakayowafikia walengwa katika chaneli yenye uwezo wa kuwahudumia zaidi ya watazamaji takribani milioni 3.5 kutoka katika nchi za Afrika. Kwa sasa hakuna kituo kinachotoa huduma hii na hivyo kuwa fursa muhimu kwa watazamaji.
Clouds TV kimataifa itarusha vipindi vya burudani, tamthilia, maigizo, ucheshi, na muziki, vyote vitakavyo kuwa vimeandaliwa kutoka nchi za Mashariki, Magharibi na Kusini mwa bara la Afrika na itapatikana kwa watazamaji walio katika Umoja wa falme za kiarabu kupitia huduma ya IPTV inayotolewa na Etisalat na Du.
Clouds TV kimataifa itarushwa kupitia mamlaka ya Abu Dhabi ijulikanayo kama twofour54, ikiungana na vituo kama FOX na CNN. Clouds TV kimataifa itaanza kurusha matangazo ya majaribio katika wiki chache zijazo kabla ya tarehe 15 mwezi June mwaka huu.

No comments:

Post a Comment